Na Shani Amanzi-Chemba.

MKUU wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga amewataka wanawake washiriki  kikamilifu katika shughuli za kiuchumi ukiwamo ujasiriamali  hasa kwa kuzingatia sehemu kubwa ya viwanda vidogovidogo vinaajiri wakina mama hasa Viwanda vya shughuli za mikono.

Odunga ametoa kauli hiyo leo wilayani hapo ambapo amesema shughuli ndogondogo za kiuchimi zinampa faida kubwa mhusika hasa akiwa mbunifu mzuri  na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli unaendelea kuwapa kipaumbele wakina mama na vijana kwa kuwapa mitaji.

"Na kwa hapa Chemba Serikali yetu inaendelea kuangalia ni namna gani wanaweza kuzidi kuwasaidia wakinamama.Ni vema kutumia muda wao kujifunza zaidi kuhusu ujasirimali una faida kubwa ,"amesema.

Kwa upande wa Mratibu wa Taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo Ulingo, Saum Rashidi amesema lengo la kwenda Chemba ni kuwafikia wanawake walioko pembezoni ili kuwawezesha katika mafunzo ya uongozi, jinsia na ujasirimali.

Amesema lengo wanapokuwa viongozi wamudu majukumu yao kama wanawake viongozi na wawe mfano wa kuigwa ndani ya jamii husika.

Amefafanua taasisi hiyo ipo jijini Dar es Salaam na ni jumuiya ya wanawake na kwamba  wanatoa mafunzo kwa wanawake wote bila kujali itikadi za vyama.

"Na kwa hapa Chemba mafunzo hayo ya ujasirimali yamefanyika ndani ya siku mbili kuanzia Juni 5 hadi Juni 6 mwaka huu katika ukumbi wa Godown, Chemba,"amesema.
MKUU wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga akizungumza kwenye semina ya Ujasirimali huku akiwataka wanawake washiriki  kikamilifu katika shughuli za kiuchumi ukiwamo ujasiriamali  hasa kwa kuzingatia sehemu kubwa ya viwanda vidogovidogo vinaajiri wakina mama hasa Viwanda vya shughuli za mikono.
Mratibu wa Taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo Ulingo, Saum Rashidi akizungumza kwenye semina ya ujasiriamali iliyohusu mada mbalimbali ikiwemo kuwafikia wanawake walioko pembezoni ili kuwawezesha katika mafunzo ya uongozi, jinsia na ujasirimali.
Baadhi ya akina Mama wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Semena hiyo ya Ujasiriamali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...