NA WAMJW-KISARAWE.

KAMBI ya upasuaji wa mabusha na matende katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe inatarajia kufanya upasuaji kwa wagonjwa wapatao 350 katika mkoa wa Pwani ili kuondoa kabisa watu wenye ugonjwa huo.

Hayo yamezungumzwa na Mratibu wa Taifa wa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD) kutoka Wizara ya Afya Dkt. Upendo Mwingira wakati alipotembelea kambi hiyo katika kufikia tamati wa mkutano wa mwaka wa kupitia,kujadili na kupanga mikakati ya kupambana na magonjwa hayo leo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

“Mpaka leo hii wagonjwa 100 wamefanyiwa upasuaji katika kambi hii ya upasuaji ya kisarawe na lengo letu ni kuwafikia wagonjwa 350 mpaka mwisho wa kambi hii itapofikia tamati kwa muda wa wiki mbili kuanzia jumatatu iliyoisha” alisema Dkt. Mwingira.

Aidha Dkt. Mwingira amesema kuwa zoezi hilo limeanza kufanywa kwenye mikoa ya lindi,Pangani na Tanga kwa kuweka kambi za upasuaji kwa wagonjwa hao na kujenga uwezo kwa wataalam wa upasuaji wa mabusha na matende wa ndani na nje ya mkoa.

Mbali na hayo Dkt. Mwingira amewataka wananchi wajitokeze kupata huduma hiyo kwani ugonjwa huo sio wa kurogwa hivyo unatibika hospitali bila ya gharama zozote na kuwaomba wajitokeze kwenye zoezi la kumeza kingatiba ya magonjwa hayo litakaloanza mwezi wa tisa mwaka huu.

Kwa upande wake Mtaalam wa upasuaji na msimamizi wa kambi hiyo Dkt. Alexander Mwerange amesema kuwa katika kufanikisha zoezi hilo wameamua kila siku kufanyia upasuaji angalau kuanzi wagonjwa 25 kwa siku ili kuendana na kasi ya kuwanusuru wagonjwa hao.

“Katika kufanikisha zoezi hili wakati mwingine wataalam inatubidi tuwafuate wagonjwa huko walipo kwani wanashindwa kufika kambini hapa kwa sababu ya usafiri hivyo tukiwapima basi tunawaleta hapa kwa ajili ya uapsuaji” alisema Dkt. Mwerange.

Aidha, Dkt. Mwerange ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa kufanikisha kambi za namna hiyo katika mikoa mbalimbali na kuwataka wananchi kutowaficha wagonjwa wa matende na mabusha bali wajitokeze ili waweze kupata matibabu hayo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...