KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu Rais John Magufuli amewavisha vyeo maafisa wa ngazi ya juu 9 wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Miongoni mwa maafisa 9 waliovishwa vyeo ni manaibu kamishna wa magereza – DCP wanne wa Jeshi hilo ambao wamepandishwa vyeo na kuwa Makamishna wa magereza, huku makamishna wasaidizi waandamizi wa Magereza -SACP watano wakipandishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna – DCP wa Jeshi hilo.

Waliovishwa vyeo kuwa Makamishna wa Magereza ni Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila, Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza Augustine Mboje, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Naibu Kamishna wa Magereza Gideon Nkana ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam.

Wengine waliovishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Julius Sang’udi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Phaustine Kasike, Mkuu wa Kitengo cha Parole pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Jeremiah Katungu ambaye ni Katibu Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo akimvalisha cheo Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila kuwa Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga kuwa Naibu wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.
Makamishina na Manaibu Kamishna wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2018. 
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt Juma Malewa akikagua gwaride maalum katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...