Na Asteria Muhozya
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amekutana na Wawakilishi wa Kampuni ya Auxin ya China ambao wameonesha nia ya Kujenga Kiwanda cha Baruti nchini.
Ujumbe wa kampuni hiyo umemweleza Waziri Kairuki lengo la kukutana naye kuwa ni kutaka kujua taratibu mbalimbali ikiwemo za Kisheria ili kujua namna ambavyo kinaweza kujenga kiwanda hicho nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Waziri Kairuki amewaeleza wawakilishi hao kuwa, endapo kampuni husika itapata fursa ya kuwekeza nchini suala la ajira kwa watanzania linatakiwa kuchukuliwa kwa umuhimu wake ili kuhakikisha kwamba watanzania wanapata ajira.
Pia, amewataka watendaji hao kusoma na kuelewa kipengele cha uwezeshaji wazawa na maeneo ambayo shughuli zao zitafanyika ili kuelewa namna ambavyo watahakikisha watanzania wananufaika na uwekezaji wao katika maeneo ambayo shughuli zao zitafanyika.
kikao hicho kimehudhuriwa  pia na  Kaimu  Kamishna  Msaidizi wa  Madini anayeshughulikia masuala ya Baruti, Chiku  Juma, Wataalam wa Wizara ya Madini na  Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kampuni hiyo inafanya shughuli kama hizo katika nchi za Congo DRC, Uganda, Namibia na Guinea.
 Waziri wa Madini Angellah Kairuki akizungumza jambo wakati wa kikao na Kampuni ya Auxin ya China ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa Kiwanda cha Baruti nchini.
  Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia masuala ya Baruti, Chiku Juma akiongea jambo katika kikao hicho. Wengine wanaofuatilia ni Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiongoza kikao kati ya Wizara ya Madini na Wawakilishi wa Kampuni ya Auxin ya nchini China.
 Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia mfano wa vifaa vinavyotengenezwa na kampuni Kampuni ya Auxin ya nchini China.
 Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati) katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Kampuni ya Auxin ya nchini China.  Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia masuala ya Baruti, Chiku Juma. Wa pili kulia ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...