NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndugu Queen Mlozi ameahidi kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uzalendo uliotukuka ili CCM ishinde katika uchaguzi mkuu wa dola mwaka 2020.
Hayo ameyasema wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa ngazi mbali mbali za UWT Zanzibar hapo Afisi Kuu CCM Kisiwandui katika ziara yake ya kwanza kujitambulisha kwa viongozi na watendaji hao.

Alisema atatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa lengo la kuimarisha taasisi hiyo ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ndani ya Umoja huo na Chama kwa ujumla.Ameeleza kwamba wanawake wa UWT wanatakiwa kuelekeza nguvu zao katika kulinda maslahi ya CCM ili ishinde kwa ngazi zote kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar katika uchaguzi Mkuu ujao.

Katibu Mkuu huyo amewashukuru viongozi viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi waliomuamini na kumteuwa kushika nafasi hiyo ya ngazi ya juu ya kiutendaji kupitia Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es saalam.

“ Viongozi na wanachama wote nakuahidini kwamba nitatumia weledi na uzoefu wangu wote kwa kuhakikisha UWT inaendelea kuwa imara na mkombozi na mtetezi mkubwa wa maslahi ya wanawake wote nchini”, alisema Queen.Akizungumza Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndugu Gaudencia Kabaka alisema ushirikiano anaoupata kutoka kwa viongozi mbali mbali wa Umoja huo na Chama unampa nguvu na imani ya kusimamia maslahi ya taasisi hiyo bila hofu.
KATIBU Mkuu wa UWT Taifa Ndugu Queen Mlozi akizungumza na viongozi na watendaji wa Umoja huo ngazi za Mikoa na Wilaya Zanzibar, Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar katika ziara yake ya kujitambulisha.


BAADHI ya Wenyeviti na Makatibu wa UWT wa Mikoa na Wilaya wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja huo Taifa.
VIONGOZI wakuu wa UWT Taifa wakiomba dua katika kaburi la Mwasisi wa Mapinduzi ya mwaka 1964 ambaye pia alikuwa ni Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza na viongozi wakuu wa UWT Taifa waliofika Ofisini kwake, Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid(kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Gaudencia Kabaka(kulia) alipofika katika Baraza hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na Wawakilishi wanawake katika Baraza hilo.
NAIBU Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma (kulia) akimkabidhi Katiba ya Jumuiya ya wawakilishi wanawake katika Baraza hilo Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Bi. Queen Mlozi (kushoto).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...