Na Hamza Temba-Dodoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza Kikosi Kazi Dhidi ya Ujangili cha Taifa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Serengeti kuwasaka watu waliohusika na mauaji ya simba tisa katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Dkt. Kigwangalla ametoa agizo hilo ofisini kwake Jijini Dodoma baada ya kupokea taarifa rasmi ya mauaji hayo ya kikatili yaliyoripotiwa hivi karibuni kwa simba hao kulishwa sumu kali katika kijiji hicho huku mmoja akikatwa miguu, mkia, ngozi ya juu ya mgongo na kuchukuliwa baadhi ya viungo vyake ambapo amesema mauaji hayo hayavumiliki kwa kuwa yana athari kubwa kiikolojia, kiutalii na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

"Bahati mbaya sana ni kuwa anapouawa simba kwa sumu hafi peke yake, inakufa familia nzima ya simba, na mara nyingi wanakufa pia wanyamapori wengine wanaodowea nyama na wanaokula mizoga. Walipouawa simba wa Ruaha hivi karibuni walikufa fisi zaidi ya 70 na ndege mbeshi zaidi ya 100, achilia mbali wadudu," amesema Dkt. Kigwangalla kwa masikitiko makubwa.
Amesema pamoja na faida kubwa za simba kwa Taifa kiuchumi, Kijiji cha Nyichoka pekee walikouwawa simba hao ni katika sehemu iliyofaidika sana na miradi ya ujirani mwema kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti."Wanyama hawa jamii ya paka wakubwa ni muhimu sana kwa kuweka mizania ya ikolojia sawa, maana wanadhibiti idadi ya wanyama wala nyasi kwa kuwala, bila hivyo hifadhi zote zinaweza kugeuka kuwa jangwa. 
Baadhi ya simba kati ya tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara
Askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikusanya miili ya simba tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara hivi karibuni kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi kubaini chanzo cha vifo vyao.
Askari wa wanyamapori wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikusanya miili ya simba tisa waliouwawa kikatili kwa kulishwa sumu, kukatwa na kuchomolewa baadhi ya viungo vyao na wananchi katika kijiji cha Nyichoka, wilaya ya Serengeti mkoani Mara hivi karibuni kwa ajili ya kuwafanyia uchunguzi kubaini chanzo cha vifo vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...