Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefuturisha wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake yaliyopo Area D Jijini Dodoma.

Futari hiyo ilihudhauriwa na wabunge mbalimbali wa chama tawala CCM na wa vyama vya upinzani wakiongozwa na Spika, Job Ndugai na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson.

Dkt. Kigwangalla aliwashukuru wabunge wote waliohudhuria hafla hiyo na kusema kuwa imelenga kudumisha upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa uliopo baina ya wabunge hao bila ya kujali mipaka ya vyama vyao hususan katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

"Nimefarijika sana kuwapokea waheshimiwa wabunge wenzangu hapa nyumbani kwangu, ninawashukuru sana kwa kuja maana shughuli ni watu, tuliandaa futari nyingi kwa ajili ya wabunge wote, sasa msingefika tungepata mtihani ni wapi pa kuipeleka. "Hafla kama hii ya Iftar inatuunganisha sisi sote bila kujali dini zetu, inajenga na kudumisha upendo, mshikamano na umoja wetu wa kitaifa bila kujali mipaka ya vyama vyetu" alisisitiza Dkt. Kigwangalla. 

Alisema zamani kulikuwa na utamaduni wa watu kufuturu nje ya nyumba zao ili wapita njia au majirani wakikuta wanafuturu nao wanajumuika, "Siku hizi tumeanza kufuturia ndani kila mtu na familia yake, basi siku moja moja kama hivi inatokea tunaamua kuukumbuka utamaduni wetu na kualikana kufuturu pamoja" alisema. 

Kwa upande Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikua mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Job Ndugai alimpongeza na kumshukuru Dkt. Kigwangalla kwa kuandaa hafla hiyo na kusema kuwa inajenga mshikamano baina ya wabunge bila kujali itikadi za vyama na dini zao. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai nyumbani kwake kwa ajili ya kujumuika na wabunge wengine kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili yao nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum, Janeth Massaburi akimuombea dua Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla katika hafla ya futari aliyoiandaa jana kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kwanye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mama Salma Kikwete kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (wa tatu kulia) akizungumza na baadhi ya wabunge kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla nyumbani kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao aliwaalika kwenye futari ya pamoja nyumbani kwake Jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...