Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

KONGAMANO la kimataifa la madaktari wa mifupa duniani limeanza kufanyika leo hadi Juni 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Ambapo linaratibiwa na Taasisi za IGOT, SIGN, OTA, OA ALLIANCE na Chuo Kikuu cha Calfonia San Fransisco cha Marekani na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.Akizungumza leo Dar es salaam Daktari bingwa wa mifupa Bill Aonga amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa na madaktari bingwa wa Mifupa wa MOI kwa kishirikiana na wakufunzi kutoka Marekani, Uingereza na Switzerland.

Amefafanua mafunzo hayo yatalenga mbinu mpya za matibabu ya mivunjiko mbalimbali ya Mifupa, magonjwa yatokanayo na ajali na namna ya kufidia kilande cha mfupa kilichopotea kutokana na ajali.Ameeleza washiriki sita kutoka Tanzania watapewa mafunzo hayo na baadaye watakuwa wakufunzi wa mafunzo hayo bila kutegemea wageni.

Pia daktari bingwa wa mifupa aliyebobea katika nyonga na kiuno Joseph Mwanga amesema idadi kubwa ya watanzania walioshiriki katika mafunzo hayo watanufaika na ujuzi waliopata utanufaisha na kuendeleza wengi.Mafunzo hayo wamelenga kuangalia namna ya kuunga mifupa na misuli mara baada ya kuchanika na kupoteza misuli.

Aidha imeelezwa taasisi ya MOI inatambulika kama kitovu cha weledi katika matibabu ya mifupa kwa muda mrefu wa paja kwa kutumia teknolojia ya kuweka chuma ndani ya mfupa.Na teknolojia hiyo hutumika zaidi duniani na hadi sasa taasisi ya MOI imefikisha wagonjwa zaidi ya 8,000 idadi ambayo haijafikiwa na hospitali yoyote duniani.

Pia mafunzo hayo hufanyika kila mwaka kwa miaka 6 mfululizo ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani na kuwapa mbinu mpya madaktari bingwa ili waweze kuendana na teknolojia ya matibabu duniani inayobadilika mara kwa mara.
Daktari Bingwa wa Uhamishaji wa ngozi Profesa kutoka Marekani,Profesa Michael Terry akizungumza na Madakri wa mifupa Duniani katika kongamano lililo fanyika leo jijini Dar as Salaam.
 Daktari Bingwa wa upasuaji Mifupa na Muhadhiri wa chuo Kikuu cha Afya Mhuhimbili,Bill Aonga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano lililo fanyika leo jijini Dar as Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Wadau mbalimbali wa afya wakiwa katika kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...