Na Stella Kalinga, Simiyu
Viongozi kutoka Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Deo Ndejembi pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi vya vijana wilayani humo wamefanya ziara Mkoani Simiyu ili kujifunza namna vikundi vya vijana vinavyotekeleza miradi yake.

Timu hiyo imefanya ziara ya siku mbili hadi Juni 08, 2018  katika miradi inayotekelezwa na vijana kwa kushirikiana na Halmashauri ambayo ni Kiwanda cha Chaki,  Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi wilayani Maswa na Mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu.

Mkuu wa wilaya ya Kongwa amesema wameamua kuja Simiyu kwa kuwa vikundi vyake vimeonekana vikifanya vizuri katika miradi yake, hivyo wamewaleta vijana wao ili wapate uzoefu na ari itawasukuma kubuni miradi yao na kujua namna bora ya kuiendesha.

"Tumeona tuje tujifunze kutoka Simiyu maana mkoa wa Simiyu umeonesha mfano wa namna vikundi vya vijana vinavyotakiwa kutekeleza miradi yake, tumeona kwenye vyombo vya habari na kwingineko mkipata sifa nyingi kutokana na miradi yenu kuonesha matokeo, nia yetu vijana waje waone wajifunze wapate hasira ya kufanya kitu cha kwao" alisema Ndejembi.
 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi (wa tatu kulia) na baadhi ya vijana kutoka Kongwa waliofika kutembelea kiwanda cha chaki wilayani humo, wakati wa ziara yao ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(kulia) akimuonesha  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi kiatu kilichotengenezwa na Kikundi cha Vijana Senani wilayani Maswa, wakati wa ziara ya Viongozi na Vijana wa Wilaya ya Kongwa kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi (kushoto) akiangalia chupa ya maziwa yanayosindikwa wilayani Meatu, baada ya kutembelea Kiwanda cha kusindika maziwa ‘Meatu Milk’ wakati wa Ziara yake na vijana wa Wilaya ya Kongwa ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi zawadi ya maziwa, mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Kusindika Maziwa wilayani humo,  wakati wa Ziara yake na vijana wa Wilaya ya Kongwa ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mmoja wa Vijana kutoka kikundi cha Maswa Family akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi na baadhi ya vijana kutoka Kongwa (wa tatu kulia) waliofika kutembelea kiwanda cha chaki wilayani humo, wakati wa ziara yao ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi (wa pili kulia) akiuliza jambo wakati alipotembea eneo la kufungashia chaki wakati alipotembelea kiwanda cha chaki wilayani Maswa, wakati wa ziara yao ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...