Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
KIKOSI cha Timu ya Taifa cha Iceland kinachoshiriki Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi, kimekuwa gumzo kubwa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji wake kuwa madaktari.Kwa kukumbusha tu idadi ya watu katika Taifa hilo la Iceland haizidi 350,000. Idadi hiyo haiwezi kuipita Wilaya yoyote ya nchini Tanzania.
Kikosi hicho chenye idadi kubwa ya madaktari katika michuano hiyo mchezo wake wa kwanza kimetoa sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Argentina, ambapo Messi alipiga mikwaju 11 (pamoja na penati aliyokosa) lakini walishindwa kupata magoli zaidi.
Katika mchezo wa kwanza kati ya kikosi hicho na Argentina nyota wa Barcelona Lionel Messi alikosa penati baada ya mkwaju wake kupanguliwa na kipa Hannes Halldorsson ambaye kitaaluma ni Producer wa masuala ya filamu.
Kikosi cha Iceland ambacho kimesheheni madaktari hadi kinaingia fainali ya kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kimecheza michezo saba, kikishinda sita na kutoka sare mchezo mmoja.
Inaelezwa mbali ya kuwa na wachezaji madaktari pia kila mchezaji anayo taaluma nyingine inayompatia mshahara mnono tofauti na soka.Pia kocha wa kikosi hicho Heimir Hallgrimsson naye ni daktari wa meno. Cha kufurahisha zaidi pia kikosi hicho kuna mchezaji ambaye ni mwanasiasa, kuna Muoka mikate na mwingine ni Mtangazaji. Kutokana na hali hiyo kikosi hicho kimekuwa fahari kubwa kwa taifa la nchi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...