Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itawasomea maelezo ya awali (PH) na kesi kuanza kuisikiliza kesi ya jinai inayowakabili viongozi wa juu wa tisa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kwa mfululizo kuanzia Juni 25 hadi 29 mwaka 2018.

Hati hiyo imekuja baada ya mawakili wa upande wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili Paul Kadushi, Wankyo Simon na Jackline Nyantori kuieleza mahakama kuwa, kesi ilikuja kwa ajili ya Ph .

Hata hivyo, Mahakama haikuweza kusoma PH kwa sababu mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Freeman Mbowe amefiwa na kaka yake na amesafiri jana kwenda kuzika Moshi.

Pia Mahakama imemtaka mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo, Mbunge wa Tarime mjini Estherher Matiko ambaye amekuwa akiripotiwa kuwa mgonjwa mara kadhaa, kuhudhuria mahakamani bila ya kukosa na asipofanya hivyo hatua dhidi yake zitachukuliwa.

Pia kesi hiyo imeshindwa kuendelea kusikilizwa ysikilizwaji wa PH leo sababu mawakili wanaowatetea washtakiwa hao Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya hawakuwepo walikuwa na kesi zingine, Kibatala ana kesi mahakama kuu. Huku Mtobesy alikuwa amehudhuria kesi Mahakama ya Afrika Mashariki Arusha na wamewakilishwa mahakamani hapo na mawakili Nashon Nkungu, Frederick Kihwelo na Hekima Mwesigwa.

Mbowe aliwakakilishwa mahakamani hapo na mdhamini wake Grayson Celestine ambaye aliwasilisha nakala ya cheti cha kifo mahakamani ili kuithibitishia mahakama, huku akiwasilishwa na mdhamini wake Patrick John ambaye alidai Matiko bado anaumwa na akawasilisha nyaraka ya mapumziko kutoka kituo cha afya ambayo inamapumziko ya siku saba kuanzia juni 21,2018 mpaka Juni 28,2018.

Hata hivyo nyaraka hiyo ilipingwa na Wakili Nchimbi kwa madai kuwa ni batili haina maelezo yanayojitosheleza ambayo yanaweza kuishawishi mahakama kuamini Matiko ni mgonjwa na anapaswa kupumzika kwa siku saba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...