THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAJALIWA ATEMBELEA OFISI ZA MPIGA CHAPA WA SERIKALI JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mitambo ya kwanza ya Mpiga Chapa wa Serikali uitwao Original Heidelberg wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam Juni 8, 2018. Mtambo huo wenye zaidi ya miaka 100 bado unafanya kazi vizuri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bw. Mohammed S. Mohammed (kulia) ambaye ni Mtalaam na mwendeshaji mkongwe wa mitambo ya uchapaji kuhusu jarada lililochapwa na mtambo uitwao Original Heidelberg wenye umri wa zaidi ya miaka 100 wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu mtambo unaochapa majarada ya serikali kutoka kwa Kaimu Mpiga Chapa wa Serikali, Bw. John Kaswalala (kushoto) wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Der es salaam, Juni 8, 2018. Mtambo huo wenye zaidi ya miaka 100 bado unafanya kazi vizuri . Kulia ni mwendeshaji wa mtambo huo, Dismas Shayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua moja ya karatasi zenye nembo na maadishi yasioonekana kwa macho ya kawaida kwenye Kitengo cha Digitali wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018. Katikati ni Kaimu Mpiga Chapa wa Serikali, John Kaswalala na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Ali Machupa. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu