Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amewataka Viongozi wa ngazi zote kuongeza nguvu katika utekelezaji wa
Sera, Sheria, Mikakati na miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa
mazingira.
Makamu wa Rais wa ameyasema hayo wakati wa Kilele cha
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yamefanyika
jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja. Ni muhimu, mipango
ya maendeleo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu
iwe na maendeleo endelevu” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa
Rais amesema kazi ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya
mazingira unahitaji ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote.
Maadhimisho ya Kimataifa yanafanyika India katika mji wa New Delhi
yakibeba ujumbe wa kuhimiza kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na
matumizi ya bidhaa za plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa
nchini Kitaifa ujumbe wa maadhimisho ni “Mkaa Gharama: Tumia Nishati
Mbadala”
Mapema leo, Makamu wa Rais alizindua ukuta wa bahari
uliopo kwenye barabara ya Barack Obama wenye urefu wa mita 920, ukuta
huo ambao umejengwa kuzuia bahari kuingia nchi kavu unakadiriwa kuwa na
maisha kati ya miaka 70 mpaka 100 kutoka sasa. Makamu wa Rais amesema
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda na
zipo faida nyingi za hifadhi na usimamizi zitakazotokana na Tanzania
kuwa na Viwanda.
Mwisho, Makamu wa Rais amesema katika
kufanikisha suala zima la uhifadhi wa Utunzaji wa mazingira mi lazima
tuifanye kila siku iwe siku ya Mazingira.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ukuta wa bahari wenye urefu wa mita 920 uliojengwa pembezomi mwa barabara ya Barack Obama mara baada ya kuizindua, mwingine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Bw.
Leonard Kushoka mfano wa hundi yenye thamani ya shiliningi za
kitanzania milioni 300 mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la
teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa mwaka 2018, wengine pichani ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
January Makamba na Mwenyekiti Mkazi wa Kampuni ya Shell Bw. Axel Knospe.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan, akisisitiza jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa
ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar
es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili
mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Alvaro
Rodriguez akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta
wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es
Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili
mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January
Makamba, akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa
ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar
es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili
mabadiliko ya tabianchi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...