Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Malawi ambalo litafanyika Julai 26 hadi Julai 27 mwaka huu mkoani Mbeya.

Kongamano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji  Tanzania(TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) pamoja na Taasisi ya Biashara na Uwekezaji ya Malawi(MITC).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika ofisi za TIC, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amesema kauli mbiu ya kongamano hilo ni "Kuimarisha Uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi" huku lengo la kongamano hilo likiwa kuwatanisha wafanyabiashara /wawekezaji  wa nchi hizo mbili ili kubaini fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji.

Ambapo amefafanua zitawezesha kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta za viwanda ,usafirishaji,utalii, uvuvi, kilimo ,madini, elimu, afya, benki, mawasiliano, tehama na biashara kwa ujumla.

Pia amesema sambamba na kongamano hilo kutakuwapo na mikutano ya wafanyabiashara (B2B), mikutano ya watendaji wa Serikali(G2G) na mikutano kati ya Serikali na wafanyabiashara (B2G) kutoka nchi hizo mbili.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali.
 Baadhi ya watendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (hayupo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Godfrey Simbeye, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Godfrey Simbeye, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Amos Makalla na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...