Na Emmanuel Masala, Globu ya jamii 

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Barabara ya Africana Kinzudi yenye urefu wa kilometer 3.3 ambayo ujenzi wake utagharimu zaidi ya Sh.Million 900.

Ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami inaenda sambamba na uwekaji wa matuta, mitaro ya maji, taa za barabarani, Calvert na alama za watembea kwa miguu ambapo itajengwa na TARURA. 

Baada ya kuzindua Barabara hiyo jana RC Makonda amefanya mkutano wa hadhara na wakazi wa Kata za Wazo na Mbezi Juu uliolenga kupatia majibu ya changamoto zinazowakabili kwenye sekta ya miundombinu, elimu, afya, maji,ardhi na usafiri.

Ambapo wakazi wa Kata hizo wamefurahia kuona kero zao za muda mrefu zimepatiwa ufumbuzi wa haraka.Pia wakati wa mkutano huo RC Makonda ameelezea miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa kwaajili ya usafiri wa treni kutoka Wazo kuelekea Mwenge, Airport na Posta ambayo itasaidia usafiri na kupunguza msongamano wa magari.

Aidha RC Makonda amewataka wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya barabara ya Afrikasana Kinzudi kushirikiana na seri kali kuhakikisha ujenzi unafanikiwa.Makonda amewata wakazi waliojenga ndani ya hifadhi ya bomba la maji kutokea Ruvu kushirikiana kwa kina na DAWASA.

Pamoja na hayo ameagiza kila mtaa kuwa na ramani ya mipango miji ili kukabiliana na migogoro ya ardhi na utapeli ambapo pia amewataka wananchi waliocheleweshewa kupatiwa vibali vya ujenzi kufika ofisini kwake Julai 1 mwaka huu.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda sambamba na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi wakiweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Africana Kinzudi jana jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi naMeya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta wakiwasili eneo la Africana kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo jana jijini Dar as Salaam.
Sehemu ya wanachi wa Africana na Kinzudi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda( hayupo pichani),alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa hadhara

Muonekano wa barabara hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Africana Kinzudi jana jijini Dar as Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...