Mamia ya wananchi na wanachama wa CCM asubuhi ya leo wamemlaki Ndg. Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipowasili kwa mara ya kwanza jijini humo kama Katibu Mkuu wa CCM na ikiwa ni kituo chake kikuu cha kazi.
Mamia ya wananchi na wana CCM walikusanyika katika uwanja wa ndege wa Dodoma na katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House).
Akizungumza na wananchi wa jiji la Dodoma waliofika kumlaki, wanachama wa CCM, viongozi wa CCM kutoka Mkoa wa Dodoma na watumishi wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Bashiru amesema amepewa dhamana kubwa na wana CCM, dhamana ya kusimamia Mageuzi Makubwa ambayo yanakirejesha Chama chetu kwa wanachama na katika misingi ambayo kwayo Chama Cha Mapinduzi kiliasisiwa.
Ndg. Bashiru amegusia kwa ufupi kazi kubwa iliyo mbele ya wana CCM kwa ujumla kuwa ni kuhakikisha kazi nzuri ya kuendelea kuhuisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya Mashina, Matawi na Kata inaimarishwa maradufu, na kwamba uhai wa Chama uende sambamba na vikao vya Chama kukaa ili kuimarisha usimamizi wa rasilimali zetu za Chama kote nchini.
Aidha Ndg. Bashiru amezuangumzia hali ya maslahi ya watumishi wa Chama Cha Mapinduzi bado si ya kuridhisha, na akatumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa CCM kwa moyo wao wa kujitolea, utii na nidhamu ya hali ya juu licha ya changamoto walizonazo.
“… Nitafanya kazi kwa bidii kuimarisha misingi ya Chama kujitegemea na tutaboresha maslahi ya watumishi, hiki ni kipaumbele namba moja na ndio Maelekezo na msimamo wa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)” amesema Katibu Mkuu wa CCM. 
 Mapokezi ya Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM Ofisi ya Makao Makuu ya CCM 
 Ndg. Bashiru Ally Kakurwa akihutubia mamia ya wananchi walifika kumlaki katika Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma
Kutoka Kulia Ndg. Rodrick Mpogolo Naibu Katibu Mkuu (Bara), Ndg. Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Mkanwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Ndg. Lubinga Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Ndg. Pereira Silima Katibu wa NEC Oganaizesheni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...