Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

KIKOSI cha timu ya Nigeria kitakuwa na kibarua kizito dhidi ya timu ya Argentina ambapo mchezo wao mwisho wa makundi utakuwa wa kuamua nani aende hatua inayofuata.

Katika mchezo huo Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akitarajiwa kuonesha maajabu ya kuivusha timu ya Argentina.

Wote wakiwa kundi D Nigeria wenye alama tatu na Argentina wenye alama moja watakutana kesho saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambapo mechi hiyo itaamua nani wa kwenda hatua ya 16 bora.Mchezo huo unaochezwa kesho Jumanne katika dimba la Saint Petersurg Jijini Moscow unaratajiwa kuwa wa ushindani mkubwa sana ambapo Argentina wenye alama moja watahitaji ushindi wa aijna yoyote waweze kufikisha alama nne na kuvuka kwenda 16 bora.

Kwa upande wa Nigeria wenye alama wakiwa wamepoteza mchezo mmoja na kushinda mmoja wao watahitaji ushindi wa aina yoyote ili kuvuka hatua hiyo wakiwa wanamuombea Croatia ashinde kwenye mchezo wake dhidi ya timu ya Iceland.Hiyvo Argentina watashuka dimbani wakiwa tayari wamepoteza mmoja na kutoka sare mmoja kukiwa na taarifa kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Jorge Sampaoli kutokupewa nafasi ya kupanga kikosi kitachovaana na The Super Eagles hata baada ya kuomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo na taifa kwa ujumla

Sampaoli alinukuliwa akisema “Kwa kweli nawajibika kwa matokeo haya lakini ilikuwa ndoto ya mashabiki kuwa timu yetu ingefika mbali, lakini haikuwa hivyo.”Kipigo hicho cha Kundi D kina maana kuwa Argentina, moja ya timu zilizokuwa zikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kabla ya kuanza kwa mashindano hayo na ambayo iliifungwa katika fainali mwaka 2014, iko hatarini kutolewa katika raundi ya kwanza ya mashindano hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...