MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Yusuph Mwenda ameishauri jamii kuendelea kudumisha amani na upendo hasa kipindi hiki ambacho Taifa linapopiga hatua za kimaendeleo chini ya Uongozi wa Rais Dk.John Magufuli.

Mwenda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kuandaa Chakula maalumu kwa ajili ya watoto wanaoishi katika Mazingira magumu wanaolelewa katika Kituo cha Malaika.Amesema katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaendelea 'kujengwa' kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo, kuna kila sababu kwa wananchi wote kudumisha amani iliyopo nchini, kama hatua ya kuungana mkono maendeleo hayo.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Taifa limeshuhudia likitekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo.Ametaja baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Reli ya Kisasa(Standard Gauge),Bwawa la kuzalisha umeme la Mto Rufiji(Stiggler's George) na kuiunganisha mikoa mbalimbali kwa barabara za lami.

"Sote tunashuhudia namna ambavyo Taifa letu linazidi kupiga hatua kuelekea mikakati ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda ifikapo 2025."Ambayo kimsingi kama watanzania tunapaswa kuipongeza,lakini ili hayo yafanyike kwa ufasaha tunapaswa kwanza kudumisha amani yetu tuliyonayo,"amesema Mwenda.


Aidha Mwenda ameiomba jamii kuwa na upendo kwa watoto wadogo hasa yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili kujiona kuwa sehemu ya familia zingine ambazo hazipo katika maisha wanayoyapitia.Amesema watoto hao ambao wengi wao wamepoteza wazazi wao wana kila sababu ya kuoneshwa upendo ili kuwajenga kisaikolojia wakati wote wanapokuwa katika maeneo wanayoelelewa.

"Hiyo itasaidia kuwapa nguvu ya kuwafikisha katika malengo yao mbalimbali ya kimaisha.Tuwapende ili wajione na wao ni sehemu ya jamii kama ilivyo kwa watoto wengine,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...