Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth kuongea na mke wake mahakamani hapo baada ya kutukumuona kwa muda wa miezi mitatu.

Ruhusa hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkuu Mkazi Mhe. Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi hilo kutokana na kutokuwa na kibali cha kumuona mumewe gerezani.

Kabla ya kutolewa kwa ruhusa hiyo, Wakili wa utetezi, John Chuma ameiomba mshtakiwa aweze kuonana na mkewe ambaye hajaweza kumuona kwa kipindi cha miaka mitatu sababu kipindi chote hicho alikuwa amefiwa na mama mkwe wake( mama wa mkewe).

"Mheshimia tunaomba mshtakiwa namba moja (Sethi) aweze kuzungumza na mke wake ikiwezekana hata kumkumbatia ili aweze kumpa pole ya kufiwa na mama yake kwa sababu bado hajapata kibali cha kuruhusiwa kwenda kumuona gerezani,"amesema. Akijibu ombi hilo Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai, alidai, " kwa sababu ni ombi anaomba kusalimiana na mkewe hapa mahakamani sina pingamizi lakini kwa magereza kuna taratibu zake na mkewe alizivuruga yeye mwenyewe."

Kutokana na majibu hayo, Hakimu Shahidi aliruhusu mshtakiwa kuzungumza na mkewe mahakamani hapo chini ya uangalizi wa askari magereza.Kesi hiyo ambayo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, imeahirishwa hadi Julai 5, mwaka huu.

Mbali na Seth mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Rugemalira ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka kumi na mawili ya uhujumu uchumi ,utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni mia tatu.
Pichani kushoto ni mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth ambaye ameruhusiwa kuongea na mke wake mahakamani hapo baada ya kutokumuona kwa muda wa miezi mitatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...