Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Uongozi wa TRC wamedhamiria kukarabati reli ya kati kipande cha kuanzia Dar es Salaam – Isaka (km970). Mradi huu umefadhiliwa na Benki ya dunia na kutekelezwa na Shirika la Reli Tanzania katika kipindi cha muda wa miaka miwili kuanzia juni 2018 hadi juni 2020. 

Lengo la uboreshaji wa reli ya kati ni kutoa usafiri wa kuaminika na kukuza upatikanaji wa huduma bora Nchini. Na maboresho hayo yatasaidia kuinua uwezo wa kubeba mzigo toka chini ya tani 13.5 za uzito wa eskeli hadi tani 18.5 kwa kufanya yafuatayo: 

I. Kutandika upya njia za reli zenye uzani wa paundi 80 kwa urefu wa kilometa 312 

II. Kufanya ukarabati wa njia ya reli iliyosalia kwa urefu wa kilometa 658 

III. Kufanyia ukarabati makaravati na madaraja 442 

IV. Kuboresha mfumo wa mawasiliano 

V. Kuboresha vituo vya kupakia na kupakua mizigo vya bandari ya Dar es Salaam, ilala na Bandari kavu ya Isaka. 

VI. Ununuzi wa vichwa vitatu vya treni (vipya) na mabehewa mapya 44 ya mizigo 

Katika kufikia malengo haya TRC itaingia mikataba 64 kati ya hiyo 32 ni ya kuajiri Washauri mbalimbali, 6 ni ya ujenzi na 24 ununuzi wa vifaa mballimbali na mikataba miwili ni ya huduma. Mpaka sasa zaidi ya 50% ya mikataba hii imeshasainiwa. 

Kupitia Mradi huu TRC pia imetengeneza mpango endelevu wa matengenezo ya miundombinu ili kufanya njia ya usafiri huu kuwa wa uhakika na kuaminika. Kuimarika kwa usafiri wa reli kutapunguza gharama za matengenezo ya barabara na hivyo serikali kuelekeza bajeti iliyookolewa kwenda kwenye huduma nyingine za kijamii. 
 Afisa maendeleo ya jamii TRC Bi Catherine Mroso, , akitoa maelezo katika kampeni ya uhamasishaji wa uelewa wa uboreshaji wa reli ya kati Dar es Salaam – Isaka katika mkutano na viongozi wa Halimashauri ya kibaha vijijini, Magindu, Mkoani Pwani. 
Wanakijiji wa Halmashauri ya kibaha vijijini, wakifuatilia kwa makini maelelezo yanayotolewa katika mkutano unaoendeshwa na wataalamu kutoka shirika la reli Tanzania - TRC Kuhusu uboreshaji wa Reli ya kati Dar es salaam- Isaka
Mratibu wa mradi wa uboreshaji wa reli ya kati Dares Salaam- Isaka, kutoka TRC Mhandisi Mlemba Allen Singo ni  akitoa maelezo katika mkutano wa wananchi wa Halmashauri ya Kibaha vijijini, Magindu, Mkoani Pwani
Muonekano wa mradi wa uboreshaji wa reli ya kati Dares Salaam- Isaka ukiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...