Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mtanzania Peter .W. Ching'ole ambaye ni mwanazuoni na mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii akiwa amehitimu shahada ya uzamili (Master's Degree) amemuandikia kitabu cha maisha ya soka ya mchezaji wa kimataifa anayekipiga nchini Ubelgiji Mbwana Samatta.

Ching'ole ameandika kitabu hicho kikiwa kinaelezewa maisha ya Samatta toka kuanza kwake kujihusisha na mpira mpaka hapa alipo sasa hivi akisaidiwa na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa mzazi wake Ally Samatta.

Kitabu hicho Kilichopewa jina la HUYU NDIYE MBWANA SAMATTA kimeweza kuonyesha Samatta akiwa na umri wa miezi tisa hadi ahapa alipo sasa hivi na kujua mwanzo wa maisha ya nyota huyo, wapi alipokulia ,familia yake, elimu aliyoipata na jinsi alivyoanza kucheza soka la mtaani mpaka soka la ushindani ambapo usajili wake kutoka African Lyon ulivyoweza kutikisa na kuzua utata mkubwa.

Ching'ole katika kitabu hicho ameelezea pia soka la kimataifa la nyota huyo, tuzo yake ya mchezajo bora wa Afrika, mafanikio ya tuzo alizopata pamoja na ubalozi wa kudumu wa maalbino na bodi ya utalii.

Kwenye kitabu hicho chenye kurasa 5t, utaona pia maisha ya soka ya baba yake na Samatta, Mzee Ally Samatta na picha mbalimbali za matukio yake ya kisoka ya zamani ikiwemo na picha za Mbwana tokea akiwa anacheza soka la mtaani mpaka hapa alipo sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...