Na Mwandishi wetu
Mchezaji wa mpira meza wa Tanzania, Sara Alidina ameingia hatua ya mashindano ya mikoa ya Kenya iliyopangwa kuanza wiki ijayo baada ya kushinda medali ya fedha katika hatua ya awali.
Sara  aambaye anasoma katika shule ya  Aga Khan Academy Mombasa, amejumuishwa katika timu ya Mvita ambayo pia inaundwa na wachezaji wawili kwa ajili ya mashindano mkoa.

Sara alianza michuano hiyo kwa vishindo baada ya kumchapa Rachel Thomas kwa seti 2-0 (11-4, 11-6) na baadaye kupata ushindani mgumu kutoka kwa Elizabeth Ochieng ambaye alianza kwa kushinda kwa 15-14 kabla ya kumbadilishia kibao na kuibuka na ushindi kwa seti mbili zilizobaki kwa  11-5 na 11-4).

Sara aliendelea kutamba katika mashindano kwa kumchapa  Christine Augustine kwa 2-0 (11-4, 11-6) na baadaye kushinda dhidi ya Maliha Haji kwa  2-0 (11-4, 11-5) na kupoteza kwa 2-0 dhidi ya Rachel Simon kwa 8-11 na 9-11.

Pamoja na kushindwa dhidi ya Rechal, Sara alifuzu hatua ya robo fainali na kushinda mechi dhidi ya Eliza Wanjiru kwa  2-0 (11-4, 11-4) na kushinda tena kwa 2-0 katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Catherine Okoth  kwa 11-4 na 11-6. Hata hivyo alikumbana na kigindi katika fainali kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Krupa Vyas kwa 11-8, 9-11 na 11-7.

Akizungumza kwa njia ya simu, Sara alisema kuwa mashindano hayo yalikuwa magumu sana na kushukuru Mungu kwa kufuzu hatua ya mashindano ya mikoa.

“Lengo ni kutwaa ubingwa pamoja na kupata ushindani mkubwa, mechi nyingi zilikuwa ngumu na hasa ukingatia kuwa nacheza na wachezaji wakubwa zaidi yangu. Hii imesababisha kuchoka na kufungwa katika hatua ya fainali,” alisema Sara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...