Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza kufanya uchunguzi na tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini na kwenye kongosho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya hadubini.

Mbali na Muhimbili kuanza kutoa huduma ya uchunguzi na kutibu wagonjwa, Kenya inatarajia kuanza kutoa huduma kama hiyo Agosti, mwaka huu.

Mpaka sasa wataalamu wa magonjwa ya tumbo na ini, wamefanikiwa kuchunguza na kutibu wagonjwa 40.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Tumbo na Ini kutoka idara ya tiba, Dkt. John Rwegasha amesema mfumo wa njia ya hadubini ni wa kisasa na kwamba unafanywa bila kufungua tumbo la mgonjwa.

Amesema kwamba mfumo wa hadibini umekuwa ukitumiwa kuchunguza na kutibu matatizo ya vivimbe na mawe kwenye ini ikiwa ni miongoni mwa mikakati wa hatua za awali wa kuelekea kwenye upasuaji wa kupandikiza ini nchini.

Pia, amesema wataalamu wa Muhimbili kwa kushirikiana na Mtalaamu Bingwa wa Upasuaji na Upandikizaji wa Ini kutoka Hospitali ya BLK India wamefanikiwa kurepea ini la mgonjwa lililopasuka ikiwa ni hatua ya msingi wa  kujenga uwezo kwa watalaamu wetu wa upasuaji.

“Tayari wataalamu wetu wa upasuaji wamefanikiwa kurepea ini lililopasuka baada ya mgonjwa kupata ajali ikiwa ni hatua ya awali kuwajengea uwezo watalaamu wetu kuelekea kwenye upasuaji mkubwa wa ini,” amesema Rwegasha.  

Akizungumzia gharama, Dkt. Rwegasha amesema kuwa gharama za kumfanyia uchunguzi na tiba kwa mgonjwa mmoja kwa matumizi ya vifaa tiba pekee ni milioni mbili na kwamba mgonjwa akitibiwa nje ya nchi ni Shs. milioni sita kwa uchunguzi na tiba ya aina hiyo kwa mgonjwa mmoja.

Amesema gharama za kupandikiza ini ni kubwa kuliko kupandikiza figo na kwamba mgonjwa mmoja anahitaji lita 20 za damu ili kufanikisha upasuaji huo.
 Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Tumbo na Ini, Dkt. John Rwegasha akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuanza mchakato wa uchunguzi na tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini na kongosho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya hadubini. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Tumbo na Ini, Dkt. Yogesh Batra kutoka Hospitali ya BLK nchini India, katikati ni Manju Sharma ambaye ni Meneja wa Uhusiano wa Kimtaifa kutoka Hospitali ya BLK. Wengine ni wataalamu wa magonjwa ya tumbo na ini.
Mmoja wa wagonjwa akipatiwa tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  tarehe 21 Juni, 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...