Dar es Salaam. Muogeleaji wa Tanzania, Natalia Ladha ametamba kufanya vyema katika mashindano ya kuogelea ya kutafuta tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya jimbo la Florida nchini Marekani yajulikanayo kwa jina la Florida Gold Coast Junior Olympic.

Natalia aliondoka nchini jana tayari kwa mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Martin County Juni 16 ambapo atajiunga na waogeleaji wa klabu ya Swimfast.

Muogeleaji huyo ambaye ni nyota kwa waogeleaji wa Tanzania wenye umri kati ya miaka tisa na 10, anashindana katika mashindano hayo makubwa matano Marekani kwa mara ya pili mfulilizo.

“Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na natarajia kufanya vyema kwa waogeleaji wenye umri kama wangu, nimejiandaa vyema katika nikiwa na makocha wangu wa klabu ya Taliss,” alisema Natalia.

Katika mashindano yam waka jana ya Miami, Natalia alishinda medali ya shaba kwa mita 50 na 100 kwa upande wa staili ya backstroke.

Natalia pia alitamba katika mashindano ya staili nyingine ambapo alitwaa medali ya dhahabu kwa mita 200 freestyle, 200 ( individual medley), 100m (backstroke),50m (butterfly) na medali ya fedha kwa mita 100 katika staili ya butterfly. Pia alishinda medali ya dhahabu kwa mita 100 katika freestyle.

Mbali ya mashindano hayo, Natalia pia atashiriki katika mashindano ya umri ya Coral Spring ambayo yataanza Juni 15 na kumalizika Juni 17 na vile vile mashindano ya Fort Lauderdale yaliyopangwa kuanza Juni 22 mpaka 24.

Vile vile atashiriki katika mashindano ya Sectionals, yaliyopangwa kuanza Julai 6 mpaka 9 ma Area championships yaliyopangwa kuanza Julai 13 mpaka 15, mjini Sunrise.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...