NA K-VIS BLOG/KhalfanSaid

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, ametembelea kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam leo Juni 8, 2018 na kuridhishwa na ubora wa mita hizo.

Alisema tatizo la mita lilikuwa ni changamoto kubwa iliyopelekea kasi ya kuwafikishia umeme Watanzania kuwa na kikwazo kwani TANESCO iliagiza mita hizo kutoka nje.

Kampuni ya Baobab Engineering System Tanzania ndiyo watengenezaji wa mita hizo za kisasa za LUKU (Smart Meters) na uongozi wa kiwanda umeahidi kuzalisha mita za kutosha ili kutatua changamoto iliyokuwa ikiikabili TANESCO kuhusu upatikanaji wa mita.

“Sisi katika kutaka shirika letu la TANESCO lifanye vizuri tumewapa maelekezo yako ndani ya Sera na mipango yetu lazima waunganishie umeme wateja wengi na moja ya component inayotakiwa ni mita, kumekuwa na changamoto ya mita kama mlivyosema, na hasa inatokana na utaratibu wa uagizaji na hata kufika kwa vifaa hivyo ilichukua muda sana, sasa uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mita hapa nyumbani ninaamini tatizo hili sasa halitakuwepo.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mgalu.

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, akiwa ameshika moja ya mita ya kisasa ya LUKU, (Smart Meter), iliyotengenezwa na kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam, wakati alipokitembelea kujionea mita hizo leo Juni 8, 2018.


Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizunguzma jambo baada ya kujionea mita hizo.
Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.
Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mimi nauliza hizi mita zinatengenezwa(zinaundwa) hapa au zinaunganishwa hapa baada ya kuagiza vipuri (parts) kutoka nje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...