Na Frankius Cleophace, Tarime

NCHI za Kenya na Tanzania zimeshauriwa kuendelea kushirikiana vema katika kupinga na kulaani vitendo vya ukeketaji kwa mtoto wa kike huku zikitakiwa kumthamini na kumpa kipaumbele katika elimu.

Ushauri huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Wazee wa Mila kutoka nchini Kenya Zacharia Ghati wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wazee wa Mila Kijiji cha Pemba kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga ambao wanapiga vita ukeketaji.Zacharia amesema kuna koo ambazo zinapatikana Tarime kwa upande wa Tanzania pia zinapatikana nchini Kenya, hivyo wote wanatamaduni moja.

" kama ni suala la ukeketaji wengine wanaenda Kenya ili kutimiza azma yao na wengine kutoka Kenya na kuja Tanzana, hivyo sasa kuna haja kubwa ya kushirikiana baina ya nchi zote mbili ili kukomesha ukeketeji,"amesema.

Kwa upande wa Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukenye Elias Maganya anasema wao kama wazee wa mila tayari wamepaza sauti zao na kudai kuwa mwaka huu hapatakuwa na ukeketaji kwa mtoto wa kike.

"Na suala la kupaka unga tutapaka watoto kuanzia miaka 15 si watoto wadogo na lengo ni kutimiza mila na ili suala litamalizika polepole kama zamani tulikuwa tunatoboa masikio."Wajaruo wanangoa Meno lakini Vyote kwa sasa vimeisha na suala la Ukeketaji litaisha lenyewe,"amesema Elias.
Zacharia Ghati Mzee wa Mila kutoka Nchini Kenya akitoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Pemba .
Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila la Wakurya na Wazee wa Mila kutoaka Nchini Kenya wakiwa katika Mkutano huo wa kutoa Elimu ya Kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
Abel Gichaine ambaye ni Mratibu wa Huduma ya Afya na Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tarime akitoa Elimu kwa Wananchi hao na kutaja madhara yanayompata Mwanamke aliyekeketwa wakati wa kijifungua na kufafanua sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.
Wangubo Mtongori Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukira Tanzania na Kenya akitoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Pemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...