Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
UONGOZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bernard Konga umekutana na uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kujadili namna ya kuboresha huduma kwa wanachama wakati wanapofika kupata huduma za matibabu hosptalini hapo.
Majadiliano ya huduma kati ya watoa huduma na Mfuko yamekuwa yakifanyika kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama wa Mfuko.
Akizungumza leo kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw.Konga amesema kuwa suala la huduma bora kwa wanachama ni kipaumbele cha Mfuko kwa kuwa wamelipia huduma hizo kabla ya kuugua.
"NHIF na watoa huduma lazima tuwe na lugha moja ya kuwapa huduma bora wanachama wetu na kama kuna tatizo linajitokeza tulishughulikie wenyewe na sio kuwahusisha wanachama wetu.
"Na kwa kufanya hivi mwanachama atapata huduma bila usumbufu wowote na itavutia wengine kujiunga na huduma zetu," amesema Bwa.Konga.
Uongozi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bernard
Konga umekutana na uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kujadili
namna ya kuboresha huduma kwa wanachama wakati wanapofika kupata huduma
za matibabu hospitalini hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...