Na Estom Sanga- TASAF

Maafisa kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza namna Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF unavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameipongeza serikali ya Tanzania kwa kutekeleza kwa mafanikio Mpango huo wenye lengo la kupambana na umaskini.

Wakizungumza baada ya kutembelea eneo la Nzasa A katika halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam, Wataalamu hao kutoka Nigeria pamoja na mambo mengine wameshuhudia Walengwa wa TASAF wakijishughulisha na uzalishaji wa bidhaa kama mikeka, vikapu ,vyungu kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.

Aidha maafisa hao kutoka Nigeria wameshuhudia namna Walengwa walivyoboresha makazi yao kwa kujenga nyumba huku wakielezwa kuwa suala la elimu na afya limepewa kipaumbele kwa Kaya za Walengwa ikiwa ni mkakati maalum wa Mpango huo kujenga rasilimali watu .Wakiwa katika eneo hilo la Nzasa A wageni hao walioko nchini pamoja na wageni wengine kutoka Sudan Kusini wamejionea namna walengwa wanavyopata ruzuku kwa njia ya simu ikiwa ni mkakati maalum wa kuboresha huduma hiyo kupitia TASAF.

Hata hivyo katika ziara hiyo kilio cha Walengwa juu ya upatikanaji wa soko la bidhaa wanazozalisha baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF kimeendelea kusikika huku walengwa hao wakiomba mfumo bora zaidi wa kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha ili waweze kunufaika vizuri zaidi.Hii leo (Jumatano)maafisa hao kutoka Nigeria na Sudan Kusini wanatembelea na kukuitana na Walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Bagamoyo kujifunza namna Mpango huo unavyowanufaisha Walengwa hao.

Serikali kupitia TASAF imefanikiwa kuandikisha zaidi ya Kaya Milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote katika Mpango huo ambao pamoja na kupata ruzuku ya fedha ya kilamwezi, lakini pia wamekuwa wakipewa mafunzo ya namna ya kukuza kipato chao kwa kuanzisha miradi midogo midogo kwenye maeneo yao.
 Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF moja ya malengo yake ni kuihamasisha Walengwa wa Mpango huo kufanya shughuli za uzalishaji mali ikiwemo ususi wa vikapo,mikeka na kuuza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. Pichani hapo juu wageni kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza na TASAF inavyotekeleza majukumu yake wakiangali bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa Mpango huo.
 Mmoja wa Wageni kutoka Nigeria akiwa ameshika kikapo alichokinunua kutoka kwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF katika eneo la Nzasa B katika kata ya Charambe wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam.
 Baadhi ya maafisa kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza namna Mfuko wa Maendeleo  ya Jamii TASAF unavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  wakiangalia bidhaa zinazouzwa na Wanufaika wa Mpango huo  katika eneo la Nzasa B wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
 Wageni kutoka nchini Nigeria wakiangalia baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- katika  mtaa wa Nzasa B kata ya Charambe wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam.

 Maafisa kutoka Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na TASAF baada ya kupata maelezo ya namna halmashauri hiyo inavyotekeleza  Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...