MFUKO wa Hifadhi ya Jamii(NSSF) umewashauri wajasiriamali nchini kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kutambuliwa na kupata mikopo.

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma wakati alipokuwa akitoa mada yake kwenye Kongamano la Wajasiriamali lilifanyika jijini Dodoma.

Chuma amesema wajasiriamali hao wakiunda na kuvisajili vikundi vyao watapata mikopo kutoka NSSF ili kukuza biashara zao.Amesema mfuko huo hautaweza kumsaidia mwananchi mmoja mmoja kwani masharti ya mikopo itatolewa kupitia vikundi au Saccos mbalimbali zilizosajiliwa.

“Lengo la mikopo hii ni kuunga jitihada za serikali katika kuwainua wananchi wa kipato cha chini kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025,”amesema.Pamoja na kupata mikopo wajasiriamali hao, watapata fursa ya kujiunga na pia na kuchangia michango katika mfuko huo jambo ambalo litawawezesha wanachama kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF.

Alitaja baadhi ya mafao hayo kuwa ni fao la Afya linalomwezesha mwanachama aliyejiunga kupata huduma za afya na mafao mengine kusaidiwa wakati wa majanga ya ajali au msiba.Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira na Vijana Anthony Mavunde amewataka wajasiriamali hao kuwa waaminifu katika kuchukua na kurejesha mikopo hiyo ili na waweze kukopeshwa.

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akionesha kadi ya uanachama wa mfuko huo alipokuwa akizungumza na wajasirimali kwenye kongamano lililofanyika ukumbi wa vijana mwisho wa wiki Jijini Dodoma 
Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akizungumza na wajasiriamali katika kongamano lililofanyika ukumbi wa vijana mwisho wa wiki Jijini Dodoma 
Wajasiriamali wakiwa kwenye kongamano uliofanyika jana Jijini Dodoma ambalo liliandaliwa na Mfuko wa NSSF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...