Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Aidha kumekuwa mafanikio katika misako kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 20.06.2018 majira ya saa 22:30 Usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya lilifanya msako huko maeneo ya Gerezani, Kata ya Ndandalo, Tarafa ya
Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kukamata vipande
tisa [09] vya meno ya Tembo na jino moja [01] la Kiboko vinavyokadiriwa kuwa
na uzito wa kilogram 30.
Thamani halisi ya meno hayo bado haijafahamika, jitihada za kuwasiliana na
Idara ya Wanyama pori zinafanyika. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea
na msako mkali kuwatafuta watuhumiwa ambao walikimbia mara baada ya
kuwaona askari. Aidha watuhumiwa wawili waliokimbia mmoja ametambulika
kwa jina [Linahifadhiwa] Mkazi wa eneo la Magereza.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi MUSSA A. TAIBU anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za siri kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi. Aidha Kamanda TAIBU anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na ujangiri na badala yake kujihusisha na shughuli halali pamoja na kulinda maliasili za nchi.

Imesainiwa na:
[MUSSA A. TAIBU - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

 Vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko vilivyokamatwa Mbeya
 Vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko vilivyokamatwa Mbeya

ACP MUSSA A. TAIBU -KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...