Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa ( kulia) akipatiwa maelezo ya maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge)’SGR’ Juni 5, 2018, usiku eneo la kambi ya Soga ,iliyopo wilaya ya Kibaha , mkoani Pwani kutoka kwa Meneja mradi wa Kampuni ya Yapi Merkezi , Kemal Artuz.

Na John Nditi, Kibaha

WAZIRI wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa ameitaka  Kampuni ya Yapi Merkezi  ya nchini Uturuki inayojenga  reli ya kisasa (Standard Gauge)’SGR’  kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro urefu wa kilomita 300 kuongeza kasi na  kufanya kazi mchana na usiku ili ujenzi huo ukamikike kwa wakati  kulingana na makubaliano ya kimkataba.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kushitukiza  Juni 5, mwaka huu ( 2018) majira ya saa tano siku kwenye  kambi ya Reli ya Mwendokasi  iliyopo Soga , wilayani  Kibaha mkoani   Pwani na kuendesha  ukaguzi hadi saa sita usiku  maeneo mbalimbali  ya  ujenzi  wa njia ya SGR.

Alisema , lengo la kufanya ziara ya kushitukiza ni  kujionea namna walivyojipata kuhakikisha kazi zinafanyika saa 24 mchana na usiku ndani ya siku saba za juma.

Profesa Mbarawa alisema , lengo ni kuona makubaliano kati ya mkandarasi na Serikali ya kukamilishwa kwa ujenzi huo ifikapo Novemba mwaka 2019 unatimizwa na wananchi kunufaika na mradi huo mkubwa.
Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa akijandaa kuelezea maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge)’SGR’ Juni 5, 2018 usiku eneo la kambi ya Soga ,iliyopo wilaya ya Kibaha , mkoani Pwani .

Hata hivyo , Waziri aliwakuta wafanyakazi na wahandisi wa mradi huo wa kiwa maeneo yao ya kazi , ambapo aliwataka watanzania walipata fursa ya kusimamia kazi hiyo kuwepo eneo la mradi kipindi chote cha saa 24 na kupangiana zamu za kazi .

Alisema , hatua hiyo itawezesha shughuli ya ujenzi iendelee kwa kasi zaidi na kwa muda wote kama ilivyopangwa  ndani yamakubaliano  na kazi hiyo inafanyika  kwa viwango vya ubora na ufanisi mkubwa.

Pamoja na hayo alitumia fursa hiyo kumkata mkandarasi wa ujenzi huo kupitia Meneja mradi  , Kemal Artuz kuogeza kasi ya ujenzi ili kufikiwa makubaliano ya kukamilishwa kwa ujenzi wa reli hiyo  kwa wakati  kuwezesha watanzania kunufaika na matunda hayo.
Kwa mujibu wa Waziri  ,njia ya reli ya mwendo kasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro  urefu wa kilometa 300 na  kati ya hizo, kilometa 205 ni eneo la njia ya reli na nyingine 95 ni za kupishana na mradi  huo  utagharimu kiasi cha Sh trrioni 2. 7.9.

“ Tayari wameanza kujenga tuta na sehemu nyingine wameweka kokoto kabla ya kuweka mataaluma  , kazi inaenda vizuri “ alisema Profesa Mbarawa na kuongeza .

“ Tuta linalojengwa linapaswa liwe na vipimo na viwango vilivyokubalika kwa pamoja  kimkataba ili reli hii ya kisasa inayotumia umeme itakuwa na uwezo wa  kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa kwa treni ya abiria ” alisema Profesa Mbarawa.

 Waziri alisema , treni ya mizigo itakuwa na uwezo wa kusafiri kwa kilometa 120 kwa saa na kubeba mizigo  tani 10,000 kwa wakati mmoja na kwa maana hiyo itaweza  kuondoa barabarani mizigo tani 20 kwa magari 500 wakati mmoja. Profesa Mbarawa alitaja kipande cha reli kingine kitakachojengwa ni kutoka  Morogoro- Makutupola chenye  urefu  kilometa 422 .

 Waziri Mbarawa alisema ,reli ya kwendo kasi itakayokuwa imejengwa kutoka Dar es Salaam hadi Makutupola itakuwa na  urefu wa  kilometa 722  na  ujenzi wake utagharimu kiasi cha  Sh trrioni 7.06.7 fedha  zinagharamiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania.
Naye Mhandisi  na Msimamizi wa mradi  wa Ujenzi wa Reli ya kisasa  , Josephat Rutaihwa alisema, kazi za ujenzi huo inaenda kwa kasi kutokana na vifaa kuwepo eneo la mradi  hadi kufikia  Juni 5, 2018 kazi zilizofanyiwa ni asilimia 13 ya ujenzi wa mradi mzima  wa kilometa  205 kutoka Dar es Salaam hadi Ngerengere.Hata hivyo alimhakikishia Waziri kuwa , kazi hiyo inakwenda kama ilivyoangwa  na kwamba mradi huo utakamilishwa  ndani ya mkataba Novemba 2, 2019.

 “ Kazi niafanyika mchana na usiku kama mlivyotukuta na mheshimiwa Waziri … na inafanyika kwa ubora na umakini na sasa tumefikia kwa baadhi ya maeneo kumwaga kokoto  na baada  kuweka mataaluma “ alisema Mhandisi Rutaihwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...