Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya JKT na Mgambo na hawana kazi wafike katika ofisi ili kushirikiana katika kuweka jiji katika hali ya usafi.

Makonda ameeleza hayo jana alipokuwa akifanya mazungumzo na viongozi wa Jeshi la kujenga taifa watokao katika Wilaya 5 za jiji, Makonda ameeleza kuwa licha ya kuweka  kila mkakati ikiwemo kutoa wito na rai kuhusu suala la usafi lakini bado jiji limekuwa chafu.

Ameeleza kuwa vijana hao watokao katika jiji la Dar es salaam wafike ofisini kwake Julai 6 ili kupata maelekezo kuhusiana na utaratibu mpya.

Kuhusiana na kazi zitakazofanywa na vijana hao Makonda ameeleza, watakaa na watendaji na kujua makampuni yanayofanya usafi na kama yanatekeleza majukumu hayo, kujua mahali ambapo wananchi wanatupa taka na kama kampuni zinazokusanya taka zinatoa risiti na kukamata kila anayetupa na asilimia 50 ya faini itakuwa sehemu ya ujira kwa vijana hao na atakayekamatwa akiwa hana fedha atafanya usafi kwa juma zima.

Aidha ameziagiza Manispaa zote ndani ya mwezi huu wa saba kila mfanyabiashara aliyepewa leseni awe na sehemu ya kutupa taka na vituo vya daladala viwe na sehemu maalumu ya kutupa ,Aidha amewataka makandarasi wote wa usafi katika ngazi zote kuwasilisha mikataba yao katika ofisi yake kuanzia Julai 4 hadi 6 ili iweze kupitiwa na tume iliyoundwa.

Pia amewashukuru wananchi na vyama mbalimbali ambavyo hujitolea kufanya usafi ili kuliweka jiji katika hali ya usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na vyombo vya habari juu ya mkakati wa kusimamia usafi katika jiji la Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...