Mwanza, 24 Juni, 2018: Msimu wa tisa wa mbio za Rock City Marathon umezinduliwa rasmi jijini Mwanza mwishoni mwa wiki hii huku wito ukitolewa kwa wadau wa utalii na michezo nchini hususani Kanda ya Ziwa kutumia mbio hizo kutangaza fursa na vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo. 

Uzinduzi wa mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA) ulihusisha pia wawakilishi wa wakuu wa mikoa yote ya kanda ya Ziwa ikiwa ni mikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara na Kagera. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw Mongella katika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall jijini humo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha alisema ipo haja ya wadau wa utalii na michezo katika kanda hiyo kuhakikisha kwamba wanayatumia vizuri mashindano hayo katika kuhakikisha fursa na vivutio vya utalii vilivyopo kwenye ukanda huo vinatangazwa ipasavyo. 

“Ndio maana serikali tunafarijika sana tunapoona sekta binafsi inajiinua na kubuni mbinu bora kabisa hasa kupitia michezo ili kuiboresha zaidi sekta hii ya utalii hususani kwa kanda yetu ya Ziwa ambayo kwa sasa ipo kwenye mabadiliko makubwa,’’ Alisema. 

Akizungumzia maendeleo ya mchezo huo Bi Tesha alisema ipo haja kwa wadau kuhakikisha wanatumia vizuri mwamko wa mkubwa mashirika na taasisi mbalimbali hapa nchini ambazo zimeamua kuunga mkono mchezo huo katika kuinua vipaji vipya. 

“Niombe sana kila kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia mchezo huu katika ngazi tofauti tofauti, idara mbali mbali na vyama mbali mbali, tulirudishe taifa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.’’ Alisema. 
 Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa msimu wa tisa wa mbio za Rock City Marathon 2018  kwenye hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa mbio hizo, Zenno Ngowi, (Kushoto kwake), Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi (alievaa suti nyeusi) pamoja na Mwakilishi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MWAA), Benjamini Nyagabona (alivaa kofia). 
 Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha akizungumza kwenye uzinduzi huo pamoja na mambo mengine alitoa wito kwa wadau wa utalii na michezo nchini hususani Kanda ya Ziwa kutumia mbio hizo kutangaza fursa na vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kanda hiyo.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mgeni rasmi ambaye Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi. Merry Tesha akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa waliohudhuria uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...