Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWEZESHAJI wa Vijana katika masuala ya maendeleo endelevu nchini Rose Mbaga amesema ikitokea akapata nafasi ya kukutana na Rais Dk.John Magufuli atamuelezea kuhusu changamoto ya ajira kwa vijana nchini.

Pia amesema katika kutatua changamoto ya ajira ametoa rai kwa Watanzania wote kushirikiana na Serikali katika kuitatua huku akisisitiza ipo haja kwa vijana kuwa na uthubutu wa kufanya mambo yanayohusu maendeleo.

Mbaga ametoa kauli hiyo jana usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akijiandaa na safari ya kwenda nchini Uingereza baada ya kutambulika kuwa miongoni mwa wanawake 100 wanaosaidia kuwainua wengine kwenye kazi za kijamii .Akiwa huko atakabidhiwa tuzo ya STAR AWARD.

"Ikitokea siku nikapata nafasi ya kukutana na Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli kikubwa nitakachomwambia ni kuhusu kuwasadia vijana na hasa wanaohitimu elimu ya juu."Kuna idadi kubwa ya vijana ambao wanahitimu elimu ya juu na changamoto yao kubwa ni ajira.Hivyo namatamani kumwambia umuhimu wa kukutana na vijana na kisha kwa pamoja tujadiliane namna ya kutatua changamoto hiyo,"amesma Mbaga.

Pia Mwanadad huyo ambaye amekuwa akijihusisha na kuhamasisha makundi ya rika mbalimbali yakiwamo ya vijana amesema anaamini kuthubutu ni jambo muhimu na hata yeye amefika hapo kwasababu ya kuthubutu na kutoa mchango wake kwa ajili ya nchi yake na nchi nyingine mbalimbali duniani.


Ametoa rai kwa vijana wa Tanzania kuhakikisha wanashiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kufafanua baada ya kumaliza chuo mwaka 2010 alikaa nyumbani kwa miaka mitatu na baadae aliamua kuanza kufanya kazi za kujitolea na sasa amekuwa mfano wa kuigwa na vijana wengine

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...