Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

UMOJA wa wananchi ujulikanao kama Rudisha Uzalendo Tanzania (RUTA) unatarajia kufanya maandamano ya amani ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kutokana na juhudi na uthubutu anaoonesha katika utendaji wake wa kazi yatakayofanyika jijini Dar es salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti wa Kamati ya maandamo hayo Charles Maselle ameeleza kuwa Juni 21, mwaka huu watafanya maandamano ya amani yasiyohusisha itikadi za vyama vya kisiasa wala dini ila wananchi wa kada zote jijini wataandamana kutoka Karume na kumalizikia katika viwanja vya mnazi mmoja na wanategemea mgeni rasmi atakuwa Rais.

Aidha amesema kuwa kama wananchi wameona ni bora kumpongeza Rais kwa sasa ili kumpa nguvu na kumtia moyo katika kazi anazofanya hasa dhamira yake ya dhati, ukweli na uthubutu katika kuleta maendeleo na wameanza kwa mkoa wa Dar es salaam na baadaye yataendelea nchini kote.

Pia Maselle ameeleza kama wananchi wameamua kurudisha uzalendo kutokana na mambo yanayofanywa na Rais kama kuboresha huduma za afya, elimu na miundombinu.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya maandamano Kigoro Athumani hayo ameeleza kuwa wanamuunga mkono Rais kutokana na juhudi na dhamira yake ya dhati katika kulipeleka taifa katika maendeleo zaidi hasa katika kuziba mianya ya rushwa  na kusimamia uadilifu katika taasisi za umma na binafsi  na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Pia amewaomba wananchi kujitokeza siku hiyo kumuunga mkono Rais kutokana na mapinduzi anayoleta bila kujali vyama wala dini.

Hali kadharika RUTA wamezindua nembo maalumu itakochapishwa katika tisheti zitakazovaliwa siku hiyo na wameomba wadau mbalimbali kutumia nembo hizo kwa kuchapa fulana na kugawa kwa wananchi siku hiyo.
 Mwenyekiti wa maandamano ya Rudisha Uzalendo Tanzania(RUTA) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya maandamano ya amani yasiyohusisha itikadi za vya vya siasa yatakayo fanyika Juni 21 mwaka huu jijini Dar as Salaam.picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.
Mwenyekiti wa kamati ya maandamano ya Rudisha Uzalendo  Tanzania  (RUTA) Charles Maselle(kulia)akiwa na wajumbe wameonesha   ya umoja huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...