Sami Hyypia veterani wa timu ya Liverpool ambaye yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered amesema kuwa mwanasoka wa mafanikio kunahitaji kazi ngumu na kujituma.
Alisema tangu utoto wake amekuwa akijituma na anaamini katika kujituma katika shughuli zinazokuinua.Alisema hayo katika hafla ya kukabidhiana vifaa kwa timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kufanyika jumamosi wiki hii, iliofanyika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Alisema kwamba kuwa juu katika soko kunatokana na mambo mawili makubwa ambayo ni kujituma na kuwa na kipaji.Alisema hata ukiwa na kipaji ukibweteka katika mazoezi na kujituma katika kuhakikisha uko fiti katika maisha ya mwanasoka huwezi kufikia ngazi za juu za uchezaji wenye kuheshimika.
Alisema pamoja na kuja kuangalia michuano hiyo amepata nafasi ya kuzungumza haja ya kukua katika soka kwa kutengeneza nidhamu inayotakiwa ya kujituma, kufanya mazoezi na kutumia kipaji katika kuimarisha usakataji soka.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akizungumza kwenye hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kulia).
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na timu (hazipo pichani) zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ gwiji huyo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kushoto) na Meneja Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered nchini, Mariam Sezinga wakipitia ratiba ya hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani).
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia wakikabidhi vifaa vya michezo kwa Afisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Mubaraka Kibarabara (katikati) ambapo Airtel ni moja kati ya washiriki 32 wa mashindano ya ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki kutoka kampuni mbalimbali wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (hayupo pichani) wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaa. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani).
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisaini ‘Autograph’ kwa baadhi ya timu zitakazoshiriki mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisalimiana na baadhi ya timu kutoka makampuni mbalimbali zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...