Na Abel Daud,KIGOMA,

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga amewataka Mahakimu wa Mkoa wa Kigoma kufanya kazi kwa Weredi pamoja na kutoa haki kikamilifu bila upendeleo ili kudumisha uaminifu kwa vyombo vya maamuzi.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema vyombo vya ulinzi na usalama nguvu yake kubwa vinategemea maamuzi kutoka kwa mahakama,nakuongeza kuwa nchi nyingi zilizo katika machafuko sehemu kubwa ni ukosefu was haki,pamoja na kutoa angalizo kuwa haki isipotolewa kikamilifu wananchi wanaweza kuchoka na kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi.

Hayo ameyasema  leo alipokuwa akifungua semina ya mafunzo ya siku moja kwa mahakimu wote wa mkoa wa kigoma, kuanzia ngazi ya mahakama ya mwanzo mpaka mahakama ya hakimu mkazi na waendesha mashtaka pamoja na Magereza.

MKURUGENZI msaidizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze amesema kuanzishwa kwa sheria hii kumepunguza mrundikano wa wafungwa katika magereza na kuongeza pato la Taifa kupitia shughuli zinazofanywa na wafungwa wenye vifungo vya nje katika taasisi za serikali ambazo zingetumia kuajili raia wengine.

Amesema hadi sasa zaidi ya wafungwa elfu kumi na sita (16) wametumikia na wanaendelea kutumikia kifungo hicho cha nje,ikitajwa kuwa wafungwa wenye vifungo vifupi kuacha kuchangamana na wafungwa wenye makosa sugu,hiyo itasaidia kupunguza uhalifu kwani pindi wawapo pamoja hujifunza tabia za waharifu hao sugu taratibu.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Manspaa ya Kigoma Ujiji Agnes Punjila amesema kuwa pamoja na sheria hii kuwa nzuri ila bado kuna changamoto kubwa hasa kwa jamii kuona kuwa sheria hiyo ni yakuwabeba baadhi ya watu na kuomba taasisi zote zinazohusika katika sheria hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii hasa kupitia vyombo vya habari.
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga  akizungumza mbele ya Washiriki wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wa tatu kulia akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...