Morogoro, June 4, 2018:SERIKALI
kwa kushirikikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF wamejipanga kutekeleza
mradi mkubwa wa Bwawa la Kidunda, hatua inayotajwa kuwa itatatua kabisa tatizo
la uhaba wa maji katika jiji la Dar es Salaam katika kipindi chote cha mwaka.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi
huo katika kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi Wilaya ya Morogoro Vijijini,
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi
Isack Kamwelwe alisema mradi huo unalenga kufanikisha adhma ya Rais John Pombe
Magufuli ya kujenga uchumi wa Viwanda.
"Tunapozungumzia ustawi wa uchumi wa viwanda
hususani kwa jiji la Dar es Salaam ni lazima kuwepo pia na upatikanaji wa
huduma ya maji ya uhakika katika kipindi chote cha mwaka. Changamoto iliyopo
sasa ni kupungua kwa kiasi cha maji katika Mto Ruvu hususani katika miezi ya
Septemba na Oktoba, hivyo mradi huu unakwenda kuhakikisha mto Ruvu unakuwa na
uhakika wa maji katika kipindi chote cha mwaka'' alisema.
Kwa mujibu wa Mhandisi Kamwene, mradi huo
utakaotekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu ni wazo la zamani likiwepo
tangu serikali ya awamu ya kwanza chini Mwalimu Julius Nyerere na kwamba
utekelezaji wake katika kipindi hiki ni mwendelezo wa adhma ya Rais Magufuli ya
kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa.
"Kukamilika kwa mradi huu tafsiri yake ni
kwamba huduma ya maji katika la Dar es Salaam inakuwa ni ya uhakika katika
kipindi cha mwaka mzima'' alisisitiza.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwene (alievaa kofia ngumu)
akifuatilia maelezo ya Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Maji
Taka Dar es Salaam (DAWASA) Prof Felix Mtalo (wa pili kushoto)kuhusu mradi
mkubwa wa Bwawa la Kidunda kutoka utakaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya
Serikali na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF alipotembelea eneo la mradi huo
katika kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi Wilaya ya Morogoro Vijijini mwishoni
mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius
Kahyarara (katikati).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwene (kulia) akibadilishana
mawazo na wadau muhimu wa mradi huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk
Stephene Kebwe (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (wa
pili kushoto) Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Attilio
Mwang'ingo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara hiyo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwene (katikati) akiongozana
akiongoza msafara wa wadau kuelekea eneo la mradi wakati wa ziara hiyo. Wengine
ni pamoja na Mkoa wa Morogoro, Dk Stephene Kebwe (kushoto) pamoja na Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba (kulia).
Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka
NSSF pamoja na DAWASA wakibadilishana mawazo wakati wa ziara hiyo.
Mchoro wa Mradi wa Bwawa la Kidunda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...