Na Frankius Cleophace Rorya

Serikali Wilayani Rorya Mkoani Mara imepiga Marufuku Jamii kumaliza kesi zinazohusu Ukatili wa Kijinsia Ukiwemo Ubakaji, Utelekezaji wa watoto wadogo, Kuchomwa Moto na Kuwatenga kwa watoto wenye Ulemavu bila kuripoti Kwenye Vyombo vya Sheria ili kuchukua hatua kali kwa wanaotenda Ukatili huo na kumaliza kiundugu jambo ambalo linazidi kunyima Mtoto haki zake za Msingi na hawatalifumbia Macho Kamwe.

Hayo yamebainishwa na Gabriel Paul ambaye ni Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya kwa niamba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.

Gabriel amesema kuwa katika Maeneo mengi vitendo vya Ukatili dhidi ya mtoto vimekuwa vikifanyika lakini jamii wanamaliza Matatizo hayo kiundugu bila kushirikisha Vyombo vya Sheria ili kulinda Mtoto dhidi ya Ukatili huo.Pia Gabriel amezitaka idara zote ikiwemo idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Mashirika Mbalimbali kuendelea kutoa Elimu kwa Jamii juu ya Madhara ya Ukatili wa kijinsia ikiwa nipamoja na kujua Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

Wilaya ya Rorya Imekuwa ikikumbwa na Changamoto ya Mimba kwa Watoto wa Shule za Msingi na Sekondari ambapo Afisa Elimu Sekondari Gabriel Paul anaeleza Mikakati ya Serikali ili kunusuru Mabinti hao huku akisema kuwa tayari watumiwa saba wamefikishwa Mahakani na wamejenga Mabweni saba na wanaendelea kuhamasisha jamii kujenga Mabweni kwa lengo la kuwapunguzia Umbali mrefu mabinti kwa ajili ya kutafuta Elimu na wakati Mwingine kushawishika na kujiingiza kwenye Mapenzi na kupata Mimba zisizojarajiwa.

Ossoro Siris ambaye ni Mwenyekiti Shirika la Shirika la Tanzaia Education Aid (TEA) amesemakuwa Shirika hilo limekuwa likiwasaidia Watoto hususani mabinti wanaotoka katika Mazingira Magumu kwa kuwalipia ada katika Shule za Serikali na Binafsi kabla ya Elimu bure lakini wa shule binafsi bado wanalipiwa.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma ya Mtoto TZ 704 Wilayani Rorya Justin Lugoye Nyanswede ameiomba Serikali kutoa bure Tauro za Watoto wa Kike Mashuleni ili kutatua Chnagamoto inayowakabili na kushindwa kuudhulia Masomo pale mabadiliko ya Mwili yanapotokea.

Aidha Watoto hao wamesema kuwa kupitia Kauli mbiu ya Mwaka huu kuwa Kuelekea Uchumi wa Viwanda Usimwache Mtoto Nyuma hivyo wameomba Wazazi kuendelea kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo Elimu na kupiga Vita Mimba za Utoto ambazo zinakatisha ndoto zao.
  Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akizungumza  katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.
 Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akipata maaelezo kwa mmoja wa Watoto Mbunifu katika sanaa ya Uchoraji na Uchingaji  katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.
 Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akipata maaelezo kwa baadhi ya Wajasiriamali kuhusua bidhaa zao mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...