SUALA la ulinzi wa siri kwa watumiaji simu janja imekua ni tatizo hasa kwa watanzania kutokana aina nyingi za security kuzoeleka na kumfanya mtumiaji siri zake kuvuja pindi simu inapoibiwa au kuwa mikononi mwa mtu asiyemuaminifu.

Na kutokana na hali hii kutowapendeza watanzania wengi hivi karibuni tumeona kampuni ya simu ya TECNO kuzalisha simu zenye mfumo mpya wa teknolojia ya security ambayo ni face id na huonekana kutumika kwenye toleo la ‘TECNO CAMON’ zilizotoka hivi karibuni. 

Lakini pia kutokana na habari zilizopo mitandaoni kwa sasa ni kwamba TECNO kuja na TECNO spark 2 kivyengine ikiwa na fingerprint pamoja na face id teknoloji ambayo ufanyaji wake kazi ni tofauti na ule wa fingerprint uliotumika katika spark za awali. Endapo kinachonekana kwenye kurasa ya tecnomobile kikawa na ukweli basi watanzania wengi watakua wamekwamuka katika tatizo hili.


Inaonekana pia madaliko hayapo tu katika upande wa security lakini pia muonekano mzima wa simu mpya za TECNO zimekuwa na wigo mpana wa kioo tofauti na spark za awali nadhani teknolojia hii mpya ni ya kuitegemaea katika TECNO spark 2 hasa ukizingatia huu ni msimu wa kombe la dunia ni wakati wako kuangalia mpira ukiwa mahala popote kupitia TECNO spark 2 

Na hivi karibu katika uzinduzi wa TECNO CAMON X na X pro nchini Nigeria kampuni ya simu ya TECNO iliweka wazi makubaliano walionayo na GOOGLE kuhusiana na simu za TECNO kuja na Android GO inayoaminika katika ufanisi wa kazi kwa haraka zaidi na utunzaji wa chaji tofauti na Android 7.0 Nougat uliotumika kwenye simu za spark.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...