Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
UNITED Bank for Africa Tanzania(UBA) imetenga Sh.bilioni 23 ambazo zitatumika kukopesha wateja wa benki hiyo na wananchi ambao wanataka kukata bima kwa ajili ya usalama wa mali zao pindi yanapotokea majanga.
Hivyo ili kufanikisha wananchi wanapata huduma hiyo ya kukatiwa bima , UBA wameamua kushirikiana na Kampuni ya Bima ya First Assurance ya jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha wanaotoa bima kubwa za aina mbalimbali.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank for Africa Tanzania Ltd Usman Isiaka amesema lengo la kutoa huduma hiyo ni kuwawezesha wananchi wenye kuhitaji bima kuipata kwa kulipia kwa awamu kwa kipindi cha mwaka mzima.
"Benki yetu itakachokuwa inafanya mteja anapokuja kwetu na kuelezea aina ya bima anayotaka kukata tunalipa fedha yote kwa kampuni ya bima ya First Assurance. Baada ya kutoa fedha hizo sisi tutakachofanya ni kumkata mteja fedha awamu kwa awamu kwa kipindi cha mwaka mmoja,"amesema.

Amefafanua benki yao pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kibenki imeona haja ya kuwarahisishia wananchi katika kupata bima hiyo kwani ni muhimu katika usalama wa mali zao ila wanamini si wote wenye kuwa na fedha yote ambayo inahitajika kukata bima kwa wakati mmoja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa  United Bank For Africa (UBA) Tanzania  Ltd Bw. Usman Imam Isiaka  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati akielezea ushirikiano walioingia  kati benki yao na Kampuni ya Bima ya First Assurance kwa ajili ya kutoa  Bima ya Insurance Premium Financing (IPF) kulia ni Bw. Bosco Bugali Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance Bosco Bugali(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati akielezea ushirikiano walioingia  na  benki  ya United Bank For Africa (UBA) kwa ajili ya kutoa  Bima ya Insurance Premium Financing (IPF) kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa  United Bank For Africa (UBA) Tanzania  Ltd Bw. Usman Imam Isiaka 
Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance Bosco Bugali  na Mkurugenzi Mtendaji wa  United Bank For Africa (UBA) Tanzania  Ltd Bw. Usman Imam Isiaka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa benki ya (UBA) na kampuni ya bima ya First Assurance mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari leo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...