Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga 

 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ,Abdallah Ulega, amesema anaandaa mpango mkakati utakaowezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda kwa kishindo katika chaguzi za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020. 
 Aidha amewatoa shaka wanaCCM wilayani hapo kwa kudai ushindi utapatikana kwani ahadi na ilani ya CCM inatekelezwa hivyo wapinzani hawana pa kupenya. Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, aliyasema hayo wakati akiongea na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mkuranga . 

 Alisema, chama kipo imara na halmashauri kuu ya CCM wilaya ndiyo jeshi namba moja la kuhakikisha ushindi huo unapatikana katika chaguzi hizo. 
 "Msikae kimya ,kila mwanachama na kiongozi kuanzia ngazi za chini ni jukumu letu kushirikiana kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali yetu na utekelezaji wa ilani"alisema. 

 Ulega alisisitiza umoja na ushikamano na kuacha kuyapa nafasi makundi ambayo hayana tija katika mustakabali wa kukiimarisha chama hicho. Alieleza anatambua changamoto ambazo bado zinalikabili jimbo hilo hivyo ataendelea kupambana nazo . 

 Ulega alisema kuwa, yapo maeneo yenye changamoto kama za miundombinu ya barabara kukatika baada ya mvua kupita ambapo tayari zipo fedha za baadhi ya maeneo ,na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa wakandarasi. 

 Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo alisema ,ataendelea na jitihada zake na kushirikiana na wadau wa maendeleo kupunguza kama sio kumaliza kero ambazo bado zipo katika baadhi ya maeneo ikiwemo elimu ,afya na masuala ya kijamii. Pia kwa kuzingatia mwezi mtukufu wa Ramadan na unakaribia kumalizika alikabidhi zakatulfitry kwa wajumbe waliohudhuria.
 Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza jambo na wajumbe wa halmashauri kuu CCM Wilaya ya Mkuranga
Mbunge wa jimbo la Mkuranga  na Naibu Waziri wa Mifugo Mhe. Abdallah Ulega akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ,Ally Msikamo kwa niaba ya wajumbe wa halmashauri kuu CCM Wilaya katika muendelezo wake wa kutambua thamani ya Chama kwa kugawana na wana CCM wenzake kidogo anachopata. Picha na Mwamvua Mwinyi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...