Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
MAHAKAM ya Hakimu Mkazi Kisutu imeuamuru upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabikili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake nane kufanyia  marekebisho katika hati ya mashtaka.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo leo mahakamani hapo baada ya kupitia mapingamizi nane yaliyowasilishwa mahakamani hapo na mawakili wa utetezi, Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya.

Hata hivyo, kutokana na  uamuzi huo Wakili, Kibatala alieleza kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo kuwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.
Katika mapingamizi hayo, upande wa utetezi waliiomba mahakama yanayowakabili kuyafuta mashtaka dhidi ya washtakiwa kwa sababu yana mapungufu kisheria ikiwamo shtaka moja kuwa na makosa mawili na washtakiwa waachiwe huru.
Ombi mbadala wa hilo, Kibatala aliomba iwapo Mahakama itashindwa kuifuta hati nzima ya mashtaka basi iyafutilie mbali mashtaka ambayo yanamapungufu kisheria.
Hata hivyo, Wakili Faraja Nchimbi akisaidiana na, Paul Kadushi walipinga madai hayo na kudai kuwa hayana mashiko kisheria.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri aikubaliana na baadhi ya hoja za upande wa utetezi, moja wapo ikiwa katika shtaka la pili, tatu, nne, tano, sita na saba yanamapungufu kisheria na kuamuru upande wa mashtaka kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka.
Baada ya kutoa uamuzi huo, Wakili Kibatala aliieleza mahakama kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo hivyo aliwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa

Wakili Kibatala alidai kuwa wanakata rufaa kwa sababu wao waliomba mashtaka hayo yafutwe lakini mahakama imeona imeamuru kuwa yafanyiwe marekebisho licha ya kuona kuwa kweli mengine ni batili.

Baada ya Kibatala kueleza hayo, Wakili wa Serikali Paul Kadushi alidai kuwa uamuzi uliotolewa wa kifanyia marekebisho hati ya mashtaka ni uamuzi mdogo ndani ya kesi, na kwa mujibu wa sheria uamuzi mdogo ambao hauwez kumaliza kesi kama huo hawawezi kuukatia rufaa.

Wakili Kibatala alisisitiza kuwa kwa kuwa mahakama imeona mashtaka hayo ni batili,  mashtaka hayo yanakufa ndiyo maana mahakama ikaamuru Marekebisho hivyo watakata rufaa. 

Baada ya mabishano hayo ya kisheria, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo atatoa uamuzi kama inaridhia ombi la akina Kibatala kukata rufaa ama la.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo Namba 112 ya 2018 ni  mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

Mbunge wa Tarime Mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk  Vicenti  Mashinji na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na  mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Wote kwa pamoja wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina.

Katika shtaka moja wapo wanadaiwa kula njama, Februari Mosi 2018 na Februari 16, 2018. Wakiwa Kinondoni Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama na wengine ambao hawapo mahakamani kwa kutenda kosa la jinai na kuendelea na mkusanyiko isivyo halali na kusababisha chuki na uchochezi wa uasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...