Na Mwandishi wetu
TAASISI ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shule ya Uchumi ya Norway (NHH) umekamilisha utafiti uliochukua miaka sita uliopelemba kama uwezeshaji wasichana kiuchumi ndio njia ya kuwezesha uzazi wa mpango.

Matokeo ya utafiti huo ‘Girls’ Economic Empowerment: The Best Contraceptive?’ umeelezwa kuja kusaidia kuelewa uzazi kwa wasichana na athari ya hali hiyo katika maamuzi yao ya kiuchumi.

Utafiti huo uliofanywa kuanzia mwaka 2013 hadi 2018, ulifanywa kufuatia programu iliyotengenezwa na Femina Hip, taasisi inayojishughulisha na kubadili tabia za vijana kwa kutumia mawasiliano.Katika programu hiyo wasichana wa sekondari walipewa mafunzo ya ziada nje ya utaratibu wao yaliyochanganywa na elimu ya afya ya uzazi, uwezeshaji kiuchumi na elimu ya maisha.

Ubalozi wa Norway jijini Dar es salaam ulifadhili sehemu ya programu hiyo.
 Maarifa yaliyopatikana kutokana na utafiti huo yanatarajiwa kuwasaidia watengeneza sera, wanazuoni na  watu wa asasi zisizo za kiserikali kutambua athari za kuwezesha au kutowezesha wasichana kiuchumi katika uzazi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa wadau na wageni waalikwa wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Wanawake Jinsia Watoto na Wazee (jinsia), Bi. Mboni Mgaza akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad akizungumza jambo wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez,  Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Wanawake Jinsia Watoto na Wazee (jinsia), Bi. Mboni Mgaza wakimsikiliza Mshehereshaji wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Shemu ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali wakishiriki kuchangia maoni wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...