Sami Hyypia veteran wa timu ya Liverpool yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered. Mchezaji huyo mwenye haiba ya aina yake aliwasili nchini Jumanne, kuhudhuria michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kuanza Jumamosi wiki hii. Akizungumza klatika mkutano na waandishi wa habari Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema benki yake imefurahjishwa sana na ujio wa mchezaji huyo wa zamani. 

“Tumefurahi sana kuwa na Sami nchini na kumshirikisha katika michuano ya tatu ya kombe la Standard Chartered . Sami pia atatumia uwepo wake kufanya kazi na timu ya vijana chini ya miaka 17– Serengeti Boys” Sami Hyypia ni mmoja wa viungo hatari ambao walivaa fulana nyekundu wakati wa utawala wa makocha Gerard Houllier na Rafael Benitez na kumfanya kuwa mmoja wa walinzi hodari barani Ulaya. 

Mchango wa Hyypia katika soka la England kulimfanya atambuliwe kwao (Finland) kwa kupewa tuzo za mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka saba. (1999, 2001, 2002, 2003, 2005, 2006 na 2008). Baada ya kusaidia timu yake dhidi ya Sheffield Wednesday hapo Agosti 7, 1999, Hyypia akawa katika mahusiano mazuri ya kisoka na Stephane Henchoz na kuwa na viungo bora wa ulinzi 2000-01. 

Aidha uchezaji wake na Jamie Carragher ulitengeneza kitu kilichokubalika kuwa ngome thabiti baada ya Liverpool baada ya kutwaa Champions League katika viwanja vya Ataturk. Hyypia ndiye aliyefunga goli la kukumbukwa sana wakati alipofunga goli dhidi ya Juve katika robo fainali. Historia ya soka, alisema mtendaji huyo wa Benki, itamweka katika eneo zuri kabisa la kibiashara mchezaji huyo ambaye wapenzi walimweka katika orodha ya kuwa mtu wa 38 kati ya watu 100 waliofanya vyema katika klabu hiyo. 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akiwa ameongozana na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Gwiji huyo wa Liverpool nchini. Wengine katika picha nyuma kutoka kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akipeana mkono na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia mara baada ya mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika na Tanzania ikiwa ni nchi yake ya kwanza kutembelea huku wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi. 
Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ujio wa Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (katikati) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...