Na Emmauel Masaka, Globu ya jamii

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini na wanachama kutekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa kufuata na kuzingatia Sheria na kanuni za vyama vya Siasa.

Taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Jaji Mutungi amesema lazima sheria za nchi kwa ujumla zifuatwe na vyama vyote vya siasa.

Amefafanua kumeibuka tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia vibaya vyombo vya habari, hususani mitandao ya kijamii kufanya vitendo au kutoa kauli ambazo zinavunja sheria za nchi.

Hivyo ametoa mwito kwa wenye tabia hiyo kuacha tabia hiyo mara moja. "Ninasisitiza kuwa viongozi wa Vyama vya Siasa wasitumie vibaya dhana ya demokrasia na uhuru wa habari."Amesema ieleweke kwamba mtu yeyote anapokiuka sheria za nchi, sheria itachukua mkondo wake bila kujali wadhifa wa mhusika katika chama cha siasa.

Amesisitiza rai yake kwa viongozi wote wa vyama vya siasa na wanachama wote wa vyama vya siasa nchini, ni wajibu wa kila mmoja wao kuelewa katika kutekeleza majukumu yao ya kisiasa wanapaswa kuheshimu sheria za nchi wakati wote ili kudumisha na kukuza demokrasia ya vyama vingi nchini. 

"Kwa kufanya hivyo pia, Viongozi hawa watalinda na kuimarisha Amani ya nchi yetu,"amesema Jaji Mutungi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...