Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez akizungumza jambo wakati na mjadala uliohusu umuhimu wa ongezeko la likizo ya uzazi kwa wazazi wenye watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Njiti), uliyoandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dae r es salaam mwishoni mwa wiki. wengine pichani kutoka kulia ni Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe, Mkurugenzi wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Ahmad Makuwani pamoja na Mdau wa maswala ya Watoto Njiti, Innocent Mungy. Warsha hiyo imefanikishwa kwa hisani ya Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Kampuni ya ASAS.
Daktari bingwa wa watoto wachanga kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Augustine Massawe akichangia mada ya umuhimu wa ongezeko la likizo ya uzazi kwa wazazi wenye watoto waliozaliwa kabla ya wakati (Njiti), iliyoandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation) katika warsha ya siku moja iliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dae r es salaam mwishoni mwa wiki.
Muongozaji wa Warsha hiyo, Chiku Lweno akitoa muongozo kwa wageni mbalimbali waliofika kwenye mjadala huo, ulioandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation).
Wadau wakifatilia mjadala kwa umakini.
maswali mengi yaliulizwa pamoja na maoni kutolewa.
Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...