Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BODI ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELB) imewachia kazi wakurugenzi sita kutokana tuhuma mbalimbali dhidi yao.

Akizungumza jana  jijini Dar es Salaam Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi wa Bodi hiyo Abdulzaq Badru amewataja waliofukuzwa ni Juma Chagonja( Mkurugenzi wa Urejeshaji wa Mikopo)na Onesmus Laizer(Mkurugenzi wa Upangaji na Ugawaji Mikopo).

Amewataja wengine ni John Elias(Mkurugenzi Msaidizi wa Ugawaji Mikopo) Robert Kibona(Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo),Heri Sago(Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Hesabu) na Chikira Jahari (Mkurugenzi Msaidizi wa Upangaji Mikopo).

Amefafanua kati ya hao waliochishwa kazi wakurugenzi ni wawili na wakurugenzi wasaidizi wanne (4). 

Amesema watumishi hao walikuwa wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo; uzembe uliokithiri, kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma 2002 na Kanuni zake, Sheria ya Bodi ya Mikopo Na. 9 ya mwaka 2004, Kanuni za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zinazo ongoza majukumu yao; na kusababisha hasara ya upotevu wa fedha za Serikali;

Badru amesema kuwa sheria na kanuni za utumishi wa Umma zinavyotaka, baada ya taratibu za ndani kukamilika.Amesema Februari mwaka huu bodi ya Wakurugenzi ambayo iliunda Kamati ya Uchunguzi iliyojumuisha wataalamu wa sheria, fedha na utumishi wa umma kwa lengo la kufanya uchunguzi na mahojiano na watuhumiwa hao. 

Amefafanua kamati hiyo imefanya kazi kwa kuwasilisha taarifa yake kwa Bodi ya Wakurugenzi kwa ajili ya uamuzi. Baada ya Uchunguzi uliofanywa na Kamati hiyo na utetezi uliotolewa na watumishi hao, Bodi ya Wakurungezi imejiridhisha kuwa watumishi hao walitenda makosa ya kinidhamu na hivyo kustahili adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazosimamia utumishi wa umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...