Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Wanachama wa Yanga kwa kauli moja wamfikia hatua ya makubaliano kwenda katika mfumo wa mabadiliko ambao utaruhusu timu hiyo kuwa Kampuni.
Yanga iliyofanya mkutano wake jana  Jijini Dar Es Salaam, ulianza kwa hotuba ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na kuwaasa wanachama wa Yanga wafanye maamuzi sahihi ili kuweza kuiweka timu yao katika dira nzuri.
Dkt Mwakyembe amesema kuwa Yanga ni alama ya ukumbusho barani Afrika kama klabu iliyoweza kusaidia upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika na bara la Afrika.
"Yanga imechaguliwa kuwa alama ya ukumbusho barani Afrika kama moja ya vilabu vilivyobeba alama ya uhuru wa Tanganyika na uhuru wa bara la Afrika, Yanga ni klabu kubwa na yenye historia yake ndania ya nchi hii , "amesema Dkt Mwakyembe.
Dkt Mwakyembe amesema uwekezaji katika klabu za mpira ni jambo lisilokwepeka na hata serikali inaunga mkono suala hilo kulingana na mahitaji yanayohitajika ili kuwa na soka la ushindani.Pia amesema wanachama waacheni kuichukulia mzaha mzaha tu na kufikia inafungwa mpaka na timu ndogo ila maamuzi yao ndiyo yatakayoamua mustakabali wa timu ya Yanga.
Pia katika mkutano huo wanachama waliweza kupinga barua ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wao Yusuf Manji na kusema kuwa bado wanamtambua kama mwenyekiti mpaka sasa hivi.Wanachama hao wamesema kuwa hawawezi kukubaliana na baria hiyo na wamemuomba arejee katika nafasi yake ya Uenyekiti wa klabu yao ambapo wka kipindi cha mwaka mmoja imekua imekaimiwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga.

Ikumbukwe kuwa Mwaka 2017, Manji aliandika barua ya kujiuzulu nafasi yake katika klabu ya Yanga ila ndani ya mwaka mzima Yanga haikuwahi kuweka mkutano wa wanachama ili kuweza kuijadili barua hiyo.Baada ya kupinga suala la kujiuzulu Manji anarejea Yanga akiwa mwenyekiti huku akisaidiwa na Makamu mwenyekiti Clement Sanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...