Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

WANANCHI wa Vijiji vya Kinyinya na Nyagwijima katika Kata ya Mgunzu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wametakiwa kushirikiana na viongozi wao kujenga nyumba za askari kwa lengo la kupunguza vitendo vya utekaji katika eneo la Kosovo wilayani humo.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema katika Wilaya ya Kakonko masuala ya utekaji yamepungua.

Ameongeza yamebaki katika maeneo machache ambayo hayafikiki kiurahisi huku akiwahimiza wananchi kutoa ushirikiano kujenga nyumba za askari ili wakae maeneo hayo na kukomesha vitendo hivyo."Wananchi wanatakiwa kujitoa kwa michango na kujitoa wenyewe kujenga, kwakuwa wanatekwa na kuporwa mali zao ni wananchi wenyewe.

"Serikali inatoa msaada mkubwa wa Kuleta maendeleo kwa wananchi, hivyo wanatakiwa kujitoa katika vijiji vyao kutokomeza vitendo hivyo.Niwaombe viongozi wa Kijiji muendelee kuhimiza suala hili la kujenga nyumba,"amesisitiza.Aidha amewataka wananchi kuwapuuza wale wote wanao wadanganya na kuwashawishi wasijitolee kuleta maendeleo.Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mgunzu Andrea Mashama amesema mkapa sasa wanaendelea kuhimiza wananchi kujitolea.

"Tumeitisha mkutano na tukakubaliana kila mwananchi kuchanga Sh.1000, hivyo wananchi wanaendelea na michango kufanikisha ujenzi wa nyumba ya Mganga na Kituo cha Afya na kufanya shughuli zingine za maendeleo kwa wananchi wote wa Kinyinya na Nyagwijima,"amesema.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi akiwamo Joachim Jolamu amesema wananchi wanaumia kwani wamekuwa waikiibiwa mazao pamoja na fedha."Tukuahidi mkuu tutahakikisha tunafanikisha ujenzi ili tuwe salama,"amesisitiza.
 Mkuu wa Wilaya hiyo,Kanali Hosea Ndagala akizungumza kwenye mkutano  mbele ya Wananchi wakati wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi .
 WANANCHI wa Vijiji vya Kinyinya na Nyagwijima katika Kata ya Mgunzu wilayani Kakonko mkoani Kigoma, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo,Kanali Hosea Ndagala kwenye mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuhamasisha maendeleo kwa wananchi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...